If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, June 15, 2017

BARRICK YAKUBALI YAISHE..IPO TAYARI KULIPA FEDHA INAYODAIWA

KAMPUNI ya Barrick Gold Corporation, ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited, imesema ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha, ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Kampuni ya Barrick Gold Corporation ya Canada, Profesa John Thornton akizungumza na wanahabari baada ya kikao na Rais John Magufuli, Ikulu Dar es Salaam jana. Kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi. (Picha na Ikulu)

Hayo ni kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited, Prof John Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Prof Thornton ambaye alisafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania, alikutana na Rais Magufuli, jana Ikulu, na mazungumzo yao yalihudhuriwa na Balozi wa Canada hapa nchini, Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi. Baada ya mazungumzo hayo, Profesa Thornton alisema kuwa kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania, yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote, ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.


Kwa upande wake, Rais Magufuli alisema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo; na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa; na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili.

Rais Magufuli alisema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa, Profesa Thornton alikubali kushirikiana na Tanzania, kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.

Chanzo: malunde.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako