If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, June 20, 2017

Binti wa Kiislamu auawa kikatili katika jimbo la Virginia nchini Marekani

Polisi nchini Marekani imetangaza kuwa msichana mmoja wa Kiislamu ameuawa katika shambulizi lililofanywa na mtu mwenye chuki dhidi ya dini ya Uislamu katika jimbo la Virginia.

Binti huyo wa Muislamu aliyekuwa na umri wa miaka 17 kwa jina la Nabra Hassanen, aliuawa Jumapili ya jana baada ya kutoka msikitini katika jimbo hilo ambapo alitekwa nyara na kupigwa na mtu mwenye chuki za kidini jimboni hapo.

Nabra Hassanen aliyeuawa

Habari zaidi zinaeleza kuwa, mwili wa binti huyo uliokotwa katika bwawa la maji eneo la Sterling mita kadhaa kutoka eneo la tukio katika jimbo hilo. Inaelezwa kuwa shambulizi hilo lilitokea wakati binti huyo alipokuwa anatokea msikitini wanapoishi Waislamu wengi akiwa pamoja na marafiki zake. 

Kijana mwenye chuki za kidini alianza kuwashambulia kwa matusi machafu na kumpiga msichana hao. Katika kujibizana kwa maneno, kijana huyo alishuka kutoka ndani ya gari yake na kuanza kumpiga na kisha kumteka nyara Nabra Hassanen na kwenda naye kusikojulikana.

Polisi wametangaza kuwa imemtia mbaroni kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Darwin Martinez Torres mwenye umri wa miaka 22.

Darwin Martinez Torres, gaidi aliyehusika na mauaji

Kabla ya hapo Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani lilitoa ripoti likitangaza kuwa, mashambulizi yanayowalenga Waislamu nchini humo yaliongezeka kwa karibu asilimia 57 mwaka jana 2016 kutoka kesi 1409 mwaka 2015 na kufikia 2213.

Kwa mujibu wa baraza hilo, ongezeko la mashambulizi hayo linatokana na matamshi ya chuki ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Waislamu na wahajiri ndani ya taifa hilo linalojinadi kuwa kinara wa haki za binaadamu duniani.

Source: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako