If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, June 5, 2017

Halima Mdee na Ester Bulaya, kutoonekana bungeni hadi 2018

Leo Jumatatu June 5, 2017 Ripoti kutoka Bungeni Dodoma zimeeleza kuwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imewapa adhabu ya kutohudhuria vikao vyote vya Bunge linaloendelea hadi Bunge la Bajeti 2018/2019 Halima Mdee na Ester Bulaya.

Wabunge hao walituhumiwa na Bunge kudharau Kiti cha Spika na kuzuia Askari waBunge kufanya kazi zao ikiwemo kufata maagizo ya Spika Ndugai kumtoa nje John Mnyika aliyekuwa akibishana naye kwa kutaka muongozo.

Kwa kuzingatia maazimio hayo ya Bunge, Wabunge hawa watarejea kwenye vikao vya Bunge katika vikao vya Bunge la Bajeti mwaka 2018 Halima Mdee na Esther Bulaya wamepewa adhabu hii baada ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwakuta na hatia ya kudharau Mamlaka ya Spika.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amebainika kuvunja kanuni ya 60 (1) (2) ikisomwa pamoja na kanuni ya 74 (1) (a) na (b) na kifungu cha 26 (d) cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296 kwa kufanya vitendo vya kudharau mamlaka ya Spika.

Wakati Esther Bulaya amebainika kuvunja kanuni ya 60 (1) (2) kanuni ya 66 (3) (a) (b) na (c) zikisomwa pamoja na Kanuni ya 74 (1) (a) na (b) na kifungu kifungu cha 26 (d) cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296 kwa kufanya vitendo vya kudharau mamlaka ya Spika.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako