If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, June 2, 2017

Human Rights Watch: Viongozi wa Kiafrika wamshinikize Rais Kabila aitishe uchaguzi wa rais

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa mwito kwa viongozi wa nchi za Kiafrika kumshinikiza Rais Joseph Kabila aitishe uchaguzi wa rais nchini humo.

Katika ujumbe huo kwenda kwa viongozi wa Umoja wa Afrika (AU), viongozi wa nchi za Afrika ya Kati na Jumuiya ya Ustawii ya Kusini mwa Afrika (SADC), Human Rights Watch limesema kuwa, viongozi wa kieneo wamshinikize Rais Kabila kwa ajili ya kuitisha uchaguzi wa rais wenye itibari sambamba na kuhitimisha hali ya sasa ya mchafukoge nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Machafuko nchini humo

Mgogoro wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliibuka baada ya kuahirishwa tarehe ya uchaguzi wa rais na kadhalika sisitiza la Rais Joseph Kabila la kutaka kuendelea kusalia madarakani nchini humo. 

Licha ya kutiwa saini makubaliano baina ya wapinzani na serikali juu ya kufanyika uchaguzi wa rais tarehe 31 mwezi Disemba mwaka huu, hata hivyo inaonekana kuwa, uchaguzi huo hautaweza kufanyika katika tarehe iliyopangwa. 

Mgogoro wa kisiasa nchini humo umeufanya hata Umoja wa Ulaya uyaweke majina tisa ya viongozi wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye orodha ya vikwazo kwa tuhuma za kuhusika na ukiukaji wa haki za binaadamu nchini humo, tangu ulipoibuka mgogoro huo.

Rais Joseph Kabila

Kwa ajili hiyo kuzuiwa mali za shakhsia hao na pia kupigwa marufuku kuingia katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa vipengee vilivyotajwa katika vikwazo hivyo vipya.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako