If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, June 11, 2017

KANU SASA YAMUONYA UHURU KUHUSU RUTO

Na GEORGE SAYAGIE

VIONGOZI wa chama cha KANU wametisha kutomuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na chama cha Jubilee ikiwa Naibu Rais William Ruto hatakoma kuwatusi wanachama wake.

Gideon Moi
Kiongozi wa Kanu Gideon Moi. Picha/MAKTABA

Mwenyekiti wa chama hicho Gideon Moi alisema chama hicho kimeitisha kikao na Rais kwa lengo la kijadili suala hilo kabla ya kuamua hatua gani watakayochukua.

“Wanasiasa wa Jubilee wakiongozwa na Naibu Rais wamekuwa wakiturushia kila aina matusi, hali ambayo huenda ikatishia ushirikiano wetu. Lakini nitakutana na Rais Kenyatta kujadili suala hilo,” akasema.

Akiongea kwenye hafla ya uzinduzi wa manifesto ya Bw Silvester Ntutu anayewania ubunge wa Narok Kusini, Bw Moi alisema, “Inavunja moyo kuona viongozi waliochaguliwa wakitishwa kiasi cha kutoweza kutoa kauli zao.

Naibu Rais anafaa kuwaheshimu viongozi wengine.” Mwenyekiti huyo wa Kanu aliongea baada ya Mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ngeno na Katibu Mkuu wa Kanu Nick Salat kuwaonya viongozi wa Jubilee dhidi ya kuwaharibia sifa viongozi wa Rift Valley.

Bw Ngeno alisema ikiwa onyo hilo halitaheshimiwa, atawashauri wakazi wa eneobunge lake kujiunga na muungano wa NASA. “Tunamwambia Uhuru amdhibiti Samoei Ruto. Ikiwa hatafanya hivyo, tutaelekeza kura zetu kwa NASA,” akasema.


Mbunge huyo mbishani alimwambia Bw Ruto kukoma kuota kwamba anaweza kushinda katika kinyang’anyiro cha urais mwaka wa 2022. “Tumeamua kwamba chaguo letu la urais 2022 ni Gideon Moi. Tunamwambia huyu bwana akome kuota kwamba atapata kiti hiki,” akasema Bw Ngeno.

Kauli sawa na hiyo ilitolewa na Bw Salat ambaye alisema wamekasirishwa na matamshi kutoka kwa wanasiasa wa kambi ya Rais Kenyatta.

Katibu huyo mkuu wa Kanu alisema itakuwa vigumu kwa Jubilee kupata asilimia 50 ikiwa Rais Kenyatta hatamdhibiti naibu wake na kumzuia kuwashambulia viongozi wa Rift Valley ambao wanaunga mkono azma yake ya kutaka achaguliwe kwa muhula wa pili.

Awali, kinara mwenza wa NASA Bw Isaac Rutto alihutubia mkutano huo na kusema kuwa mrengo huo umeweka mikakati murwa ya kuzuia wizi wa kura.

“Mwaka huu tutazima njama za wale wote ambao lengo lao ni kuvuruga kura kwa kuendesha udanganyifu,” akasema gavana huyo wa Bomet. Rutto pia aliisuta serikali kutokana na ongezeko la bei ya bidhaa za chakula.

“Hatuna haja na unga wa mahindi wa Sh90 uliotolewa na serikali ya Jubilee. Kile Wakenya wanahitaji ni uimarishaji wa sekta ya kilimo ili waweze kumudu bei ya mahindi huku wakulima nao wakinufaika,” akasema Gavana Ruto.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako