If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, June 16, 2017

KARUA: IEBC IPEWE NAFASI KUFANYA KAZI YAKE

Na SAMMY WAWERU'

MWANIAJI wa kiti cha ugavana Kirinyaga kwa chama cha Narc Kenya Bi Martha Wangare Karua amewasihi wanasiasa na vyama mbali mbali vya kisiasa nchini kuipa nafasi tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) wajibu wake wa kusimamia na kuendesha uchaguzi bila masharti yoyote.

Bi Martha Karua
Kiongozi wa Narc Kenya Bi Martha Karua akihutubu katika kituo cha Mfumo wa Vyama Vingi vya Kisiasa (CMD) katika hoteli ya Intercontinental, Nairobi Februari 16, 2016. Picha/ANTHONY OMUYA

Bi Karua amesema IEBC imetunukiwa mamlaka ya kuendesha uchaguzi na katiba akionya msukumo wa kisiasa inaopokea kutoka kwa wanasiasa na vyama mbali mbali huenda ukayumbisha uchaguzi na yumkini kuzua ghasia Agosti 8.

"Kuongea matamshi yasiyo na msingi wala breki dhidi ya IEBC ni kuhatarisha uchaguzi mkuu ujao. Mimi mwenyewe siwezi tamka maneno ninayosikia baadhi ya wanasiasa wakiyamwaga kwa umma, ninazungumza kama mwanasheria ambaye amehudumu katika idara ya sheria," akasema Bi Karua Ijumaa Gichugu Kaunti ya Kirinyaga akifanya kampeni kusaka kura achaguliwe gavana Agosti 8.

Matamshi ya Bi Karua yanajiri wakati ambapo IEBC inakabiliwa vikali na mrengo wa upinzani National Super Alliance (NASA), NASA ikitaka zabuni ya kuchapisha karatasi za kupiga kura inayoendelea katika kampuni ya Al-Ghurair, Dubai isitishwe na ipuuziliwe mbali.

NASA aidha inasema wasimamizi wa kampuni hiyo wana uhusiano wa karibu na familia ya Rais Uhuru Kenyatta, wakieleza wasi wasi huenda zabuni hiyo inayogharimu sh2.5 bilioni ikawa nguzo ya wizi wa kura Agosti 8.

Bi Karua amesema madai hayo ambayo sasa yamekuwa mada ya mazungumzo kwenye vyombo vya habari, aliyasoma kwenye magazeti na kuyaskia kwenye redio na runinga.


"Mimi hayo niliyaskia kwenye redio na runinga, pia nimeyasoma kwenye magazeti. Wakati mtu anasema mambo kama hayo anafaa awasilishe ushahidi mezani," akasema.

"Ushahidi uwasilishwe mezani tuushuhudie, matamshi kama hayo yanahatarisha amani na uchaguzi mkuu ujao ambapo yakiendelea kuzua mjadala yatazua ghasia," akaonya Bi Karua.

Mbunge huyu wa zamani wa Gichugu na ambaye alihudumu kama waziri wa sheria nchini chini ya serikali ya Rais Mstaafu Mwai Kibaki, ameeleza imani yake kwa tume ya IEBC kuwa imejipanga na itaendesha uchaguzi mkuu ujao kwa njia ya uhuru, haki na uwazi.

"Ninafikiria hadi sasa tume ya IEBC imefanya kazi nzuri na iko wazi kwa kila inachofanya. Naomba wanasiasa na vyama tuunge mkono IEBC ili iweze kuendesha uchaguzi kwa njia ya amani na ifaayo," akashauri Bi Karua.

Tume ya IEBC inaongozwa na mwenyekiti wake Wafula Chebukati.

Mrengo wa NASA kupitia mkurugenzi mkuu wa maandalizi ya uchaguzi Musalia Mudavadi, unashikilia sharti zabuni hiyo iliyopewa kampuni ya Al-Gurair usitishwe na kupokezwa kampuni nyingine.

Alhamisi Bw Mudavadi akiandamana na vinara wengine wa NASA jijini Nairobi walisema hawana imani na zabuni hiyo na kwamba uchaguzi ujao utakuwa wa uhuru na haki endapo itasitishwa na kukabidhiwa kampuni nyingine ya kuchapisha karatasi za kupiga kura wanayoiamini.

NASA inaongozwa na Raila Odinga wa ODM akisaidiwa na mgombezi mwenza Kalonzo Musyoka wa Wiper Party. Madai ya NASA yamepokelewa kwa hisia tofauti na viongozi wa Jubilee.

Asuta Nasa

Rais Uhuru Kenyatta Ijumaa akiandamana na Naibu wake William Ruto katika Kaunti ya Kericho kusaka kura za kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili na ya mwisho, alisuta mrengo wa NASA kwa kutoridhishwa na kila tume ya IEBC na makamishna wake huku akirejelea shinikizo zilizochangia mwenyekiti wa awali IEBC Isaack Hassan kuondoka ofisini.

"Walianza kwa kutangaza kuwa hawakuwa na imani na makamishna wa tume ya IEBC iliyokuwa inaongozwa na Isaack Hassan kama mwenyekiti. Sio eti ilikuwa na makosa, lakini haja yao ilikuwa kuzindua njama ya uchaguzi usifanyike," akasema Rais.

Rais Kenyatta alisema tetesi za NASA zinaegemea kwa msingi wa kugawana serikali baada ya uchaguzi wa Agosti 8 iwapo watabwagwa.
"Hakuna uhalali uliopo ndani ya tetesi zao ila wanacholenga ni muda wa kujiandaa uishe, awamu ya serikali kuwa mamlakani kikatiba iishe ili waje sasa watwambie tugawane serikali," akasema Rais.

Bi Martha Karua ambaye ndiye kiongozi wa chama cha Narc Kenya ashauri malumbano ya kisiasa yaliopo kuhusu IEBC hayafai, ila tume hii iwachiwe majukumu yake iyaendeshe kwa amani.

"Tume ya IEBC ilibuniwa kisheria kwa hivyo ipewe nafasi iendeshe kazi yake bila msukumo wowote. Malumbano ya kisiasa yaliyopo yataitatiza kuendesha kazi yake," akasema.

Hata hivyo Bi Karua anayewania ugavana Kirinyaga ameeleza imani yake ataibuka mshindi Agosti 8 kwa kuwabwaga wapinzani wake.
"Nilipopewa wizara ya maji na sheria nilifanya kazi kwa moyo mmoja na kuafikia malengo niliyopewa. Nilimudu wizara hizo mbili na kuleta maendeleo, hivyo basi rekodi yangu ya utendakazi ni safi na bora na ya kupigiwa mfano. Ninaamini nikiwa kiongozi wa kaunti nitafanya bora zaidi," akasema akiuza sera zake kwa wananchi.

Kwenye kinyang'anyiro cha ugavana Kirinyaga, Bi Karua atatoana kijasho na aliyekuwa Waziri wa Ugatuzi Bi Anne Waiguru anayemezea mate kiti hiki kwa tiketi ya chama cha Jubilee.

Gavana wa sasa Kirinyaga Joseph Ndathi pia atakuwa debeni kuwania kuhifadhi kiti chake kama mgombeaji wa kujitegemea baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mchujo Jubilee mwezi Aprili na Bi Waiguru.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako