If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, June 16, 2017

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa: Israel inaunga mkono magaidi

Katibu Mkuu wa Umoja wa maraufa amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unatoa himaya na uungaji mkono kwa makundi ya kigaidi likiwemo la Jabhat al-Nusra linaloendesha harakati zake huko nchini Syria.

Antonio Guterres amesema kuwa, imekuja katika ripoti maalumu ya kikosi cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la miinuko ya Golan ya Syria kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel kuna wakati umekuwa ukituma misaada na hata kuwa na uratibu wa moja kwa moja na makundi ya kigaidi ya nchini Syria.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kuwa, hadi sasa kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa kimesajili kesi 16 za mawasiliano baina ya utawala wa Kizayuni wa Israel na makundi ya kigaidi.

Silaha wanazopelekewa magaidi nchini Syria

Wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akieleza hayo, kuna nyaraka za wazi zinazoonyesha kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukiyasaidia makundi ya kigaidi nchini Syria yanayofanya mauaji dhidi ya raia wasio na hatia kwa kisingizio cha kutaka kuindoa madarakani serikali ya Rais Bashar al-Assad.

Baadhi ya ripoti zinaonyesha kuwa, hata magaidi wanaojeruhiwa katika mapigano yao na wanajeshi wa Syria wamekuwa wakipatiwa matibabu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel).

Licha ya hayo na hata kuweko ripoti za Umoja wa Mataifa zinazothibitisha wazi juu ya misaada ya Israel kwa makundi ya kigaidi, umoja huo umekuwa ukitosheka tu na kutoa ripoti za kukemea kitendo hicho; kwani hadi sasa haujachukua hatua za maana dhidi ya utawala huo ghasibu.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako