If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, June 25, 2017

Kauli ya Rais Magufuli kuhusu wanafunzi wanaopata mimba yawakasirisha wanawake

Wanawake wamekasirishwa na matamshi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ya kupiga marufuku kurejea shule wasichana wanaopata ujauzito hata baada ya kujifungua.

Wanaharakati mbalimbali wa masuala ya wanawake wamekosoa kauli hiyo na kumtaka Rais Magufuli kuomba msamaha kwa matamshi hayo. Aidha baadhi ya wanaharakati wa masuala ya eneo wameitaka serikali ya Tanzania kutazama upya sheria inayomfukuza shuile msichana mwanafunzi anayepata mimba.

Shirika moja la wanawake barani Afrika limemtaka Rais Magufuli aombe msamaha na wakati huo limewataka wanawake kusimama na kuipinga sheria hiyo ya Tanzania.

Sheria iliyopitishwa mwaka 2002 nchini Tanzania inaruhusu kutimuliwa wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni.

Wanafunzi wasichana wa Shule ya Sekondari ya Weruweru ya Moshi Tanzania

Sheria hiyo inasema kuwa, wasichana wanaweza kufukuzwa shuleni kwa ''makosa yanayokiuka maadili na ndoa''.

Ni kwa muda sasa makundi ya haki za wanawake yamekuwa yakiishinikiza serikali ya Tanzania kubadilisha sheria hiyo, ingawa mpaka sasa juhudi hizo hazijazaa matunda.


Mjadala kuhusiana na sheria hiyo umeibuka tena nchini Tanzania baada ya hivi juzi Rais Magufuli kunukuliwa katika mkutano wa hadhara akiwaonya wasichana wa shule kwamba ''unaposhika mimba mambo yako yamekwisha''.

Rais wa Tanzania aidha alisema, wanaume wanaowatia mimba wasichana wa shule pia nao wanapaswa kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 30 na kuweka nguvu zao walizozitumia kuwatunga mimba wasichana hao kulima wakiwa jela.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako