If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, June 21, 2017

KDF: KURIA AMSHANGAA RAILA

Na MWANGI MUIRURI

MBUNGE wa Gatundu Kusini, Moses Kuria Jumatano 'amemcheka' Raila Odinga kwa kudai kuwa Jeshi linatumika kuandaa mikakati ya wizi wa kura.

KDF
Wanajeshi wa KDF awali. Picha/MAKTABA

Kauli ya Kuria inajiri huku Raila akiwa tayari ametoa hotuba akiwa ofisi za Okoa Kenya, Nairobi ambapo muungano wa National Super Alliance (Nasa) umezindua mpango wa Adopt a Polling Station unaonuia kulinda kura, hasa za urais 'zisichakachuliwe' kuvuruga uhalali wa matokeo.

“Raila wa Odinga huchekesha mtu. Eti sasa anasema Jubilee inataka kutumia jeshi la taifa kuiba kura zake. Akisema hivyo 'amevaa' sura ya kujiangazia kama mwathiriwa wa njama hiyo. Huyu ni mwigizaji hodari ambaye hakugundua na kuifanyia kazi talanta yake akiwa mchanga,” amesema Kuria.

Kuria ambaye ni mbunge wa Gatundu Kusini ambaye yumkini hajawahi kunukuliwa akiwa na lolote jema kumhusu Odinga amesema, “Huyu Odinga amesahau kuwa amehusishwa na jaribio la mapinduzi la 1982 lililosababishia idara ya jeshi hasara kubwa. Wakati huo serikali mamlakani ilikuwa ya Rais Mstaafu Daniel Arap Moi.”

Hata hivyo Raila ameshawahi kujitetea awali akisema kuwa hakupatikana na hatia. Aidha, alitiwa gerezani bila hata kusomewa mashtaka.

Kuria akiwa katika msafara wa kumlaki rais akizulu Murang’a Jumatano kusaka kura amesema kuwa “alisababishia wengi wa wanajeshi kufutwa kazi, wengine wakatorokea mataifa jirani na hatimaye wengine wakahukumiwa kunyongwa.”


Kuria alisema kuwa “kile kinachomsumbua Odinga kwa sasa ni majuto kuwa alisababishia idara hiyo dosari kuu katika mtazamo wa kinidhamu na ambapo hadi sasa katika madaftari ya idara hiyo Odinga ameorodheshwa kama adui wa nidhamu ya jeshi la taifa.”

Alisema kuwa kwa sasa Odinga angekuwa anajiimarisha kwa kuwarai wapiga kura wake wasimame naye na wampigie kura “badala ya kugeuza vita vyake kwa idara ambayo haitakuwa katika kivumbi hicho cha Agosti 8, 2017 kama mpinzani wa urais.”

Aidha, amemtaka Odinga aelewe kuwa “kura za hapa Kenya hupigwa hadharani na zikiwa zimesimamiwa na wadau wengi. Huwa unalia tu umeibiwa kura ili kujitakasa aibu ya kujaribu kwa bidii za mchwa kutwaa mamlaka bila ufanisi.”

Amesema kuwa “Odinga angekuwa tayari amekubalika kuwa kiongozi wa kitaifa iwapo angejithibiti tabia yake ya kushambulia taasisi na jamii kiholela kiasi kwamba huishia kujipa nembo ya aliye na hisia kali za kisasi moyoni mwake dhidi ya karibu kila mtu asiye wao kisiasa.”

Katika hali hiyo, “ningemshauri Odinga ajiandae kuanguka katika kura ijayo kwa kuwa jinsi tunavyokaribia uchaguzi huo mkuu, ndivyo anazidi kuimarika katika kujikwaa ulimi na pia kimikakati.”

Akasema: “Katika kipindi cha wiki moja sasa, Odinga amejikwaa kwa kusema wageni Kajiado wafurushwe makwao, wamiliki wa mashamba Laikipia wapokonywe mashamba hayo na sasa kuwa jeshi ni la maafisa wezi wa kura. Anayeanguka kura hujulikana kwa mienendo na tabia sawa na hii Odinga anajipata akijihusisha nayo.”

Raila ametishia kuelekea mahakamani kupinga zabuni ya kuchapisha karatasi za kura. Anataka kampuni tofauti itafutwe.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilitoa tenda hiyo ya Sh2.5 bilioni kwa kampuni ya Al-Ghurair, Dubai.

Nasa wanadai wakurugenzi wa kampuni hiyo ni wandani wa Rais wa Kenya aliye mamlakani Uhuru Kenyatta wa Jubilee Party.

Source: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako