If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, June 15, 2017

KENYA: HATUTAZIMA INTANETI WALA MAWASILIANO AGOSTI 8 - WANGUSI

Na CAROLYNE AGOSA

MAMLAKA ya Mawasiliano Kenya Jumatano imetoa hakikisho kuwa haitazima intanenti siku ya uchaguzi mkuu.

Francis Wangusi
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (CA), Francis Wangusi akihutubia wanahabari jijini Nairobi, Februari 17, 2017. Picha/ OMAR KIBULANGA

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo CAK, Prof Francis Wangusi, alisema kuwa huduma za mtandao zitakuwepo kama kawaida Agosti 8 Wakenya watakapopiga kura kuwachagua viongozi wapya nchini.

“Hatuna nia ya kuzima intaneti wala mawasiliano wakati wa uchaguzi,” Prof Wangusi aliambia wajumbe katika kongamano la kitaifa kuhusu uchaguzi. Kongamano hilo lililoanza Jumatatu lilikamilika jana katika jumba la mikutano la KICC mjini Nairobi.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kampuni zote tatu za mawasiliano ya simu nchini – Safaricom, Airtel na Telkom (zamani ikijulikana kama Orange) – zimehusishwa ili kuhakikisha kuwepo kwa mtandao kwa minajili ya kusambaza matokeo ya kura kwa njia ya kielektroniki.

Aidha, Prof Wangusi alisema simu zitakazotumiwa kutuma matokeo zitastahili kusajiliwa ili kuonyesha kituo cha kupiga kura ambako matokeo yatatoka, na hivyo kuimarisha uadilifu.

Kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Prof Abdi Guliye, alisema kuwa vifaa 45,000 vya kutambua wapiga kura (BVR) vitatumika Agosti 8.


Tayari 11,000 vilitumika katika zoezi la kuthibitisha maelezo ya wapiga kura lililokamilika Ijumaa iliyopita.

Vifaa vingine zaidi vya habari na mawasiliano (ICTs) vinaendelea kuwasili nchini; vya hivi punde vikiwa ni seva mbili za kuhifadhi data zilizowasili wiki hii, moja itakayotumika kama hifadhi kuu na nyingine hifadhi mbadala.

Kamishna huyo alisema kuwa IEBC inajizatiti kuzuia matatizo yaliyosababisha kufeli kwa vifaa vya BVR wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Alieleza Prof Guliye: “Changamoto ambazo zimekumba zabuni za ununuzi wa vifaa ndizo zimechelewesha kuwasili kwa vifaa hivyo. Mwaka 2013 vifaa vilifika kwa kuchelewa sana ikawa vigumu kwa wasimamizi wa uchaguzi na wananchi kuvifanyia majaribio kabla ya siku ya kura.

“Hata hivyo, vifaa vyote vitakuwa tayari kutumwa katika vituo vya kupiga kura wiki mbili kabla siku ya kupiga kura Agosti 8.”
Kamishna huyo alitahadharisha kuwa teknolojia pekee haitahakikisha kuna uchaguzi wa kuaminika.

“Tunahitaji maafisa wa uchaguzi kuwa na ujuzi wa kuzitumia na, muhimu, zaidi imani ya wananchi. Wakenya hatuaminiani kabisa; na hiyo ndiyo sababu kuu ya wananchi kushinikiza teknolojia itumike kuendesha uchaguzi kwa njia ya kielektroniki.

“Hii ni tofauti na demokrasia zilizokomaa kama Ufaransa tunakonunua vifaa hivi ya BVR, ambako hawatumii teknolojia yoyote katika uchaguzi wao,” akasema prof Guliye.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako