If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, June 23, 2017

KENYA: USIYOYAJUA KUHUSU MAUJI YA MUCHAI

Na RICHARD MUNGUTI

SHEMEJIYE aliyekuwa Mbunge wa Kabete George Muchai aliyeuawa kinyama Alhamisi alilia katika mahakama kuu hata ikabidi kesi hiyo iahirishwe kwa muda wa dakika 20.

Samuel Wachira Muchai na  Esther Mumbi Gitau
Samuel Wachira Muchai na Esther Mumbi Gitau wakiwa kizimbani Aprili 28, 2016. Picha/PAUL WAWERU

“Itabidi tuahirishe kesi hii kwa muda wa dakika 20 shahidi huyu atulie,” Jaji James Wakiaga anayesikiza kesi ya mauaji dhidi ya washukiwa saba aliamuru.

Kesi hiyo iliahirishwa ndipo Bi Judy Njoki Ngigi atulie.

Bi Ngigi alishindwa kutoa ushahidi aliposema kwamba mkewe marehemu alimpigia simu “ lakini hakujibu.”

Akasema : “ Dada yangu alimpigia mumewe simu lakini hakujibu. Alipigia walinzi wake wawili hawajibu pia. Alimpigia dereva naye hakujibu. Tuliamua kurudi nyuma kisha tukapata wote wanne wameuawa.”

Alipofikia sehemu hiyo ya ushahidi , Bi Ngigi alishindwa kuendelea na ushahidi ndipo mahakama ikaamuru kesi isitishwe kwa muda atulie.

Awali Bi Ngigi alisema alisikia milio minne ya risas nzito.

Bi Ngigi anayefanya biashara Afrika kusini , alimweleza Jaji Wakiaga kwamba, usiku ule Muchai aliuawa walikuwa wanatoka katika sherehe katika eneo la Westlands.

Bi Ngigi alisema , marehemu pamoja na walinzi wake wawili na dereva wake waliuawa kinyama.

“Nilisikia milio minne ya risasi lakini sikushtuka kwa vile kule Afrika kusini ninako ishi kila siku kunasikika milio kila siku.


Bw Muchai aliuawa pamoja na walinzi wake wawili.

Washukiwa saba wamekanusha walimuua Muchai. Walioko kizimbani ni Eric Muyera Isabwa almaarufu Chairman, Raphael Kimani Gachii almaarufu Kim, Mustafa Anyonyi, Stephen Lipapo almaarufu Chokore, Simon Wambugu Gichamba, Jane Wanjiku Kamau almaarufu Chiko na Margaret Njeri Wachori.

Wote walikanusha walimuua Muchai.

Bi Ngigi alisema Muchai aliuawa karibu na Jengo la Nyayo jijini Nairobi. Alimweleza Jaji Wakiaga yeye na mkewe marehemu walikuwa wanasafiri kwa gari moja na walisikia milio ya risasi wakiwa katibu na jengo la Emporium karibu iliyoko katika makutano ya barabara za Koinange na Kenyatta Avenue jijini Nairobi.

Alisema Muchai akiuawa aluoijsimama kununua magazeti.
Kesi inaendelea.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako