If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, June 26, 2017

Korea Kusini: Pyongyang iwaachilie huru watu wetu na Wamarekani inaowashikilia

Waziri Mkuu wa Korea Kusini ameitaka serikali ya Korea Kaskazini kuwaalichilia huru raia wa nchi hiyo na wale wa Marekani ambao wanashikiliwa na serikali ya Pyongyang.

Lee Nak-yon ametoa ombi hilo baada ya kufariki dunia mwanafunzi mmoja raia wa Marekani aliyekuwa akishikiliwa katika jela za Korea Kaskazini. Ikumbukwe kuwa wakati Otto Warmbier mwanafunzi huyo wa Marekani alipoachiliwa huru kutoka katika jela huko Korea Kaskazini, alikuwa amepoteza fahamu.

Otto Warmbier mwanafunzi wa Marekani, wakati alipotiwa jela Korea Kaskazini

Kitendo cha mwanafunzi huyo kupoteza maisha muda mfupi baada ya kuachiliwa huru na Pyongyang, kimeamsha hasira za jamii ya kimataifa ambazo zimeitaka Korea Kaskazini kuweka kando miradi yake ya nyuklia na kuheshimu haki za binaadamu. Otto Warmbier aliyezuiliwa nchini Korea Kaskazini kwa muda wa miezi 17, alifariki dunia baada ya kufikishwa Marekani. Hadi sasa raia sita wa Korea Kusini wanaendelea kushikiliwa katika jela za Korea Kaskazini kwa makosa tofauti. 

Tarehe 19 mwezi huu Rex W. Tillerson, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani aliiomba serikali ya Pyongyang kuwaachilia huru raia wengine watatu wa Marekani ambao wapo katika jela za nchi hiyo ya Asia. Katika hatua nyingine Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini ametoa mwaliko kwa Korea Kaskazini wa kushiriki katika michezo ya olimpiki itakayofanyika wakati wa msimu wa baridi kali mwaka 2018 katika mji wa PyeongChang, nchini Korea Kusini.

Askari wa Korea Kaskazini


Rais Moon Jae-in ametoa mwaliko huo katika sherehe za ufunguzi wa mashindano ya taikondo (Taekwondo) ya ubingwa wa dunia mwaka 2017 ambayo yanafanyika katika mkoa wa Jeollabuk-do nchini Korea Kusini. 

Katika sherehe hizo rais huyo amesema kuwa, ikiwa wanamichezo wa Korea Kaskazini watashiriki michezo ya olimpiki mwaka 2018 itakuwa ni hatua kubwa ya kuboresha urafiki na usalama kati ya nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako