If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, June 5, 2017

KURA ZA RIFT VALLEY NI ZAKO RAIS, GIDEON AAMBIA UHURU

Na SAMMY WAWERU

SENETA wa Kaunti ya Baringo Gideon Moi amemhakikishia Rais Uhuru Kenyatta kuwa atavuna kura chungu nzima kutoka Bonde la Ufa.

Seneta wa Baringo Gideon Moi
Seneta wa Baringo Gideon Moi awali. Picha/MAKTABA

Seneta huyu ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha tangu jadi cha Kenya African National Union (KANU) amesema amejitolea mhanga kupigia Rais Kenyatta debe Bonde la Ufa almuradi aone amechaguliwa katika uchaguzi mkuu ujao Agosti 8, 2017.

"Mimi ni Mkalenjin, jana (Jumamosi) nilikuwa huko (maeneo ya Bonde la Ufa) na mambo si mabaya kwake Rais Kenyatta," amesema Gideon Moi akihutubu Limuru, kaunti ya Kiambu.

Mei chama cha KANU kilitangaza rasmi kumuunga Rais Kenyatta Agosti 8 na kuahidi kumfanyia kampeni.

"Sisi KANU tuliamua 'tuko ndani' na Rais Uhuru Kenyatta. Tuliamua kwa sababu ya kitu kimoja; tunataka Uhuru amalize kutekeleza miradi yake ya maendeleo aliyotuahidi tunayoona inabadilisha maisha ya Wakenya. Tumpe hiyo nafasi tena Agosti 8 abadilishe maisha yetu," amesema Gideon Moi.

Seneta huyu wa Baringo ambaye ni mwanawe Rais Mstaafu Daniel Arap Moi amewataka wananchi kumpigia Rais Kenyatta kura kwa wingi akisema anathamini uongozi wa Uhuru.

"Kila kura iko na maana, tusichezee hii kura ya mwaka huu wa 2017. Tumeona vile wenzetu (NASA) wamejipanga, kila kura tujue ina maana. Kiambu, Nyeri, Bonde la Ufa na maeneo mengine nchini tuko tayari kumchagua Rais Kenyatta."


"Hata mimi mniwekee kura yangu iwe ndani," akaongeza akijifanyia kampeni ili kuwania tena kiti chake cha useneta Kaunti ya Baringo.

Seneta Gideon na Naibu wa Rais William Ruto wamekuwa wakionyesha ubabe wao kutaka kuonekana ni nani aliye na ushawishi mkubwa kwa jamii ya Wakalenjin kati Bonde la Ufa.

Mwenyekiti huyu wa KANU hata hivyo ametaka wananchi wadumishe amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu ujao.

"Zimesalia takriban siku 60 tuingie kichinjioni, tujue uchaguzi utakuja na upite. La muhimu tufahamu Kenya itasalia ilivyo hakuna mahali itaenda. Tusiweke mbele mambo mengi yasiyo na msingi, yaliyo muhimu ni maisha yatakayokuja. Maisha ya mbele ndiyo tunafaa tufikirie, kwa hivyo tudumishe amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi," akawarai wananchi.

Kauli ya Seneta imeenda sambamba na matamshi ya Rais Uhuru Kenyatta akihutubu kwenye kanisa la Kingdom Seekers Nakuru leo Jumapili baada ya misa akikamilisha ziara yake ya siku tatu Kaunti ya Nakuru kwa lengo la kupigia debe chama cha Jubilee dhidi ya uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 8.

"Tunaomba Mungu atupe amani na umoja tunapojiandaa kushiriki uchaguzi mkuu ujao. Muombe amani iendelee kudumishwa msimu huu wa siasa," amesema Rais Kenyatta.

Ushindi

Baada ya Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto kichaguliwa mwaka wa 2013, Jubilee iliandaa maombi ya kitaifa katika uwanja wa Afraha Nakuru ili kushukuru Mwenyezi Mungu na wananchi kwa ushindi wao.

Rais kwenye hotuba yake ametaja Kaunti ya Nakuru kuwa kaunti inayowafungulia na kuwafungia awamu ya uongozi pindi Jubilee inapochaguliwa.

"Ahadi zetu tulipokuwa hapa (Afraha Nakuru) miaka 5 iliyopita ilikuwa amani itawale nchi, tuliapa taifa hili halitamwaga damu tena kwenye uchaguzi wowote kama ilivyoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwakwa wa 2007. Mungu ni mkuu amani imedumu na kuenea kwenye utawala wetu wa Jubilee. Kaunti hii ya Nakuru ndipo 'Yesu' huja kuomba kuwepo na amani anapoanza kazi na anapoikamilisha, tunaomba Mungu atupe amani ili tuweze kuafikia malengo yetu," akasema Rais Kenyatta akiongeza kuwa kuna haja ya jamii zote nchini kuheshimiana na kuishi kwa amani.

Ghasia zilizotokea mwaka wa 2007/2008 zilipelekea zaidi ya wananchi 1,300 kuaga na maelfu ya watu kufurushwa kutoka makwao.

Kando na chama cha KANU kutangaza kumuunga Rais Kenyatta kuchaguliwa tena Agosti, chama cha Maendeleo Chap Chap (MCC) kinachoongozwa na Gavana Alfred Mutua, chama cha Narc Kenya cha Martha Karua, PNU cha Gavana Peterunya na DP ni miongoni mwa vyama ambavyo pia vilitangaza kumuunga rasmi Rais Kenyatta Agosti 8.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako