If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Thursday, June 29, 2017

Maandamano ya kuunga mkono marekebisho ya katiba ya Mali

Makumi ya maelfu ya wananchi wa Mali jana waliandamana huko Bamako mji mkuu wa nchi hiyo wakiunga mkono mpango wa kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo.

Waandamanaji karibu elfu sita wanaounga mkono kufanyika kura ya maoni kuhusu katiba ya nchi hiyo jana walikusanyika katika uwanja wa michezo wa Bamako kufuatia wito uliotolewa na jumuiya za vijana karibu 20 za nchi hiyo.

Wiki iliyopita Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali aliakhirisha hadi wakati mwingine kura hiyo ya maoni iliyokuwa imepangwa kufanyika tarehe 9 Julai kutokana na baadhi ya pande kupinga kitendo cha kumpatia Rais mamlaka zaidi.

Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali


Upande unaounga mkono kufanyika kura hiyo umesema kuwa upo udharura wa kuifainyia marekebisho katiba ya Mali ili kutekeleza makubaliano ya amani yaliyosainiwa katikati ya mwezi Juni mwaka juzi.

Katiba ya Mali inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kufanikisha utekelezaji wa makubaliano ya kusaka amani ya nchi hiyo yaliyosainiwa kati ya serikali, makundi yanayobeba silaha yaliyo karibu na serikali na waasi wa zamani wa Tuareg wa kaskazini mwa nchi. Baraza la Seneti na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali zinatarajiwa kuasisiwa iwapo katiba ya Mali itafanyiwa marekebisho.

Source: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako