If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, June 28, 2017

Mataifa 30 yanashiriki maonyesho ya biashara ya sabasaba nchini Tanzania

Makampuni kutoka nchi 30 duniani yanatarajiwa kushiriki katika maonyesho makubwa ya kibiashara yanayojulikana kama sabasaba nchini Tanzania, ambayo hufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam.

Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa mgeni rasmi Julai Mosi katika ufunguzi wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayosimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yaliyoaanza rasmi leo Juni 28 hadi Julai 8, 2017 yakishirikisha makampuni toka nchi zipatazo 30.

Charles Mwijage Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Tanzania amesema kuwa, maonesho ya mwaka huu yamelenga zaidi kusaidia wajasiriamali wadogo ili kuifikisha Tanzania katika uchumi wa viwanda.

Sehemu ya Uwanja wa Maonyesho ya Kibishara ya Sabasaba Dar es Salaam

Amesema kuwa, kaulimbiu ya mwaka huu ni "Ukuzaji wa biashara kwa maendeleo ya viwanda" kwa sababu tunaamini biashara ndiyo inayokuza viwanda na bila kuuza hakuna ukuaji wa viwanda.

Waziri mwijage ameongeza kuwa, lengo hasa la maonesho hayo ni kuwapa fursa wafanyabiashara kuonesha bidhaa zao na si kuuza, ili wanapomaliza maonesho wapate wateja na fursa pana zaidi za kibiashara.

Awali akimkaribisha Waziri Mwijage katika viwanja vya maonyesho hayo hapo jana, Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka aliwataka washiriki watumie maonyesho hayo kutangaza bidhaa zao badala ya kufikiria kuuza, lakini pia wabadilishane ujuzi na uzoefu na wafanyabiashara wa kimataifa.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako