If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, June 12, 2017

RAILA HANA KISASI NA JAMII YA AGIKUYU, ACHAGULIWE - NG’ARU

Na WANDERI KAMAU

KINARA wa NASA Raila Odinga hana kisasi chochote na jamii ya Agikuyu, amedai mbunge mmoja.

Odinga amsalimia Rais
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amsalimia Rais Uhuru Kenyatta katika hafla ya mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha David Mwiraria Aprili 22, 2017. PICHA/ PSCU

Akizingumza na kituo kimoja cha redio Jumapili jioni, mbunge maalum katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Bi Mumbi Ng’aru alisema kwamba ni wakati jamii hiyo ibadilishe dhana kumhusu Bw Odinga, akisema kuwa hana nia yoyote mbaya dhidi yake.

Aidha, Bw Ng’aru, ambaye anawakilisha chama cha ODM katika bunge hilo, alisema kwamba amekuwa rafiki wa karibu wa Bw Odinga, ambapo hajaona sababu zozote za Bw Odinga kuuchukia jamii hiyo, kaama vile imekuwa ikidaiwa na wanasiasa wengine.

“Bw Odinga ni mtu mpenda watu. Hana chuki wala kisasi chochote na jamii ya Agikuyu. Hiyo ni dhana ambayo imekuwa ikienezwa na viongozi wa Mlima Kenya kwa manufaa yao wenyewe,” akasema Bi Ng’aru.

Mbunge huyo ambaye aliwahi kuhudumu kama meya wa mji wa Thika alimmiminia sifa Bw Odinga, akisema kwamba Wakenya wanapaswa kushukuru kwani ndiye alikuwa mwasisi wa mfumo wa ugatuzi.


Alisema kwamba miradi mingi ya Serikali ya Jubilee ilianzishwa na Bw Odinga, wakati akihudumu katika iliyokuwa Serikali ya Muungano chini ya Ris Mstaafu Mwai Kibaki.

“Ingawa tunaishukuru Jubilee kwa kukamilisha miradi hiyo, hawapaswi kumsahau Bw Odinga kama mwasisi mkuu,” akasema.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako