If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, June 26, 2017

RAILA: VITENDAWILI VYANGU VINAIWASHIANI JUBILEE?

Waziri Mkuu Raila Odinga
Mwaniaji urais wa muungano wa NASA Raila Odinga. Picha/MAKTABA

Na LEONARD ONYANGO

MWANIAJI wa urais wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga amewataka wanasiasa wa Jubilee kukoma kuzungumzia vitendawili vyake kama 'ajenda' katika mikutano yao.

Akizungumza Jumapili katika Uwanja wa Busia, Kaunti ya Busia, Bw Odinga alidai Jubilee 'wameishiwa na sera na sasa wanatumia vitendawili vyake kujipigia debe.'

"Wale majamaa (Jubilee) kila waendapo wanasema Raila, Raila ati yule jamaa wa vitendawili. Mimi nauliza vitendawili vyangu je, vyawawashiani?" akasema Bw Odinga.

Kinara wa NASA anaonekana kumjibu Naibu Rais William Ruto ambaye amekuwa akimrejelea kama 'Yule Jamaa wa Vitendawili'.


Bw Odinga amekuwa akitumia vitendawili kila anapohutubia mikutano ya kisiasa.

Jumapili, katika mkutano wa Busia, Bw Odinga alitega: "Kitendawili, alitembea usiku na kulipokucha alijikuta hana nguo na akaaibika! Huyo ni nani?"

Umati: Jubilee
Raila: Mmekosea ni mchawi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako