If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, June 24, 2017

RAIS KENYATTA AMHAKIKISHIA RAILA USALAMA WAKE

Na MWANGI MUIRURI

Rais Uhuru Kenyatta akiwa katika Kaunti ya Nyeri Alhamisi kuwarai wenyeji wamuunge mkono akisaka awamu ya pili mamlakani katika kura kuu ya Agosti 8, 2017 alimhakikishia kinara wa Nasa, Raila Odinga usalama wake.

Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta akihutubu awali. Picha/BILLY MUTAI

RAIS Uhuru Kenyatta akiwa katika Kaunti ya Nyeri Alhamisi kuwarai wenyeji wamuunge mkono akisaka awamu ya pili mamlakani katika kura kuu ya Agosti 8, 2017 alimhakikishia kinara wa Nasa, Raila Odinga usalama wake.

Alisema kuwa Odinga hafai kuwa na lolote la kumtia kiwewe kuhusu hatima yake ya sasa nay a baadaye “kwa kuwa serikali yangu itakupa askari wa kutosha wa kukulinda na pia tukupe pensheni ya kukuweka bila shida yote ukistaafu kutoka kwa siasa.”

Rais alisema kuwa “hakuna mtu atagusa wewe.”

Haileweki moja kwa moja kama huu ni ujumbe wa kumpa afueni Odinga kutokana na hatari inayoning’inizwa machoni mwake na wakereketwa wa Jubilee kuwa atashtakiwa kuhusu madai ya uchochezi.

Pia, Odinga hivi majuzi alituma ombi kwa serikali ya Jubilee la kutaka aongezewe ulinzi wa maafisa wa polisi wa kiwango cha juu na magari ya kusafiria.

Rais Kenyatta alijitosa katika sakasaka zake za kura za eneo hilo kupitia kujiangazia kama aliye na utaifa ndani ya huduma yake kwa Wakenya kinyume na Odinga ambaye alimwangazia kama wa kuzua uhasama wa kijamii.


Akirejelea mada ya Jubilee ya kumkaanga Odinga kufuatia 'kuteleza' ulimi kwake akiwa Kajiado Rais alisema, “Wakati yeye yuko Kajiado akipigia debe uhasama wa kijamii, sisi tuko hapa tukipeana hatimiliki za mashamba.”

Rais alitangaza kutimizwa kwa ahadi yake ya maadhimisho ya Madaraka Dei katika uwanja wa Kabiru-ini ya kuwatuza maskwota wa eneo hilo hati miliki za kuwapa uthabiti wa kuwa wenyeji wa Nyeri halali.

“Sio tu watu wa hapa Nyeri tunapea vyeti hivyo muhimu. Tumewapa hata watu wa jamii zingine wakiwa katika eneo hili kwa kuwa wao ni Wakenya na wanakoishi ndio kwao,” akasema.

Rais Kenyatta aliahidi kuwa uwanja wa Ruring’u utakarabatiwa ili uzinduliwe rasmi katika kipindi cha miezi saba ijayo.

Aidha, alitangaza kuwa ufadhili wa ujenzi wa hospitali ya Kansa katika Kaunti hiyo utajengwa katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Kimathi, kinyume na ahadi ya awali kuwa ingejengwa katika uwanja unaohifadhi hospitali kuu ya Nyeri.

Rais alisema badiliko hilo ni kufuatia “uhaba wa ardhi katika uwanja huo wa hospitali ya Nyeri na badala yake imeamuliwa na wadau kuwa ijengwe katika chuo hicho ili pia iwe ni hospitali na taasisi ya kutoa mafunzo kwa makurutu wa kimatibabu.”

Rais Kenyatta alisema tayari serikali yake imejishindia ushirika wa ufadhili kwa ujenzi wa hospitali hiyo kutoka serikali ya Hungary.

Pia, alisema kuwa barabara kuu ya Thika Superhighway itarefushwa kutoka Thika, ipitie Kaunti za Murang’a, Kirinyaga, Nyeri, Laikipia na Isiolo, hatua ambayo alisema kuwa itarahisisha usafiri na uchukuzi wa bidhaa.

Alitangaza kuwa ufadhili wa harakati hizo utatoka kwa benki ya maendeleo barani Afrika (ADB).
Huku akionya wenyeji kuhusu uzembe wa kupiga kura, alisema angetaka sana wajitokeze wakamtimue Odinga kwa kura ndani ya debe “kiasi kwamba kabla ya saa tatu asubuhi awe na ufahamu kuwa anaelekea nyumbani.”

Kenyatta alisema kuwa anategemea wapiga kura wa Nyeri kumpa guu mbele katika kivumbi hicho na akawataka wajitume kwa dhati kumshikilia.

Naibu wake, William Ruto ambaye anaonekana kuwa ndiye amewajibishwa juhudi za kuwarai wao katika ngome zao muhimu kuchagua tu wawaniaji wa Jubilee alisema kuwa “Nyeri safari hii msituchezeshe karata ya pata potea na kura zenu. Chagueni rais Kenyatta na watu wake wa mkono ndani ya Jubilee.”

Alisema kuwa uthabiti wa serikali ya UhuRuto awamu ya pili utategemea sana idadi ya wagombezi wa Jubilee ambao watafaulu kuchaguliwa.

Hata hivyo, katika maeneo kadha ya Othaya na Mathira, UhuRuto walikumbana na upinzani mkali kuhusu mito yao ya upigaji kura mtindo wa suti, hii ikiwa ni katika Kaunti ya tatu ya Mlima Kenya kukumbana na ukaidi huo.

Tayari, maeneo kadha ya Kaunti ya Laikipia, Kiambu na sawsa Nyeri yamekataa kuchangamkia wito huo wa kupigia kura Jubilee kuanzia Urais hadi kwa diwani.

Maeneo hayo yamemhakikishia rais kuwa kura ya Urais ni yake, bora tu wawachiwe uhuru wa kujiamlia katika nyadhifa hizo zingine.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako