If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, June 22, 2017

Ramadhani Ulimwenguni "BENIN''

Kutoka Niger, leo tunavuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Benin.

Benin ni nchi ndogo iliyoko Afrika ya Magharibi ikichungulia bahari ya Atlantik. Kabla ya mwaka 1975 nchi hiyo ilikuwa ikijulikana kwa jina la Dahomey (Dahome). Inapakana na Togo, Nigeria, Burkina Faso na Niger.

Mji Mkuu: Porto-Novo. Lakini mji mkubwa kabisa ni Cotonou (Kotonoo), na huu pia ndio mji mkuu wa kibiashara, kama ilivyo Dodoma na Dar es Salaam kwa Tanzania.

Benin ilikuwa chini ya Ukoloni wa Ufansa mpaka ilipojipatia uhuru wake mwaka 1960, na ina idadi ya watu zaidi ya milioni 10. Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini lugha za Fon na Kiyoruba zinazungumzwa kwa wingi nchini humo.

Idadi ya Waislamu: Takwimu rasmi za serikali zinasema kuwa idadi ya Waislamu ni 24%, lakini Waislamu wenyewe wanasema kuwa idadi yao haipungui 55%, wakidai kuwa wao ndio walio wengi.

Ramadhani Nchini Benin:

Ramadhani inapowaisili, Benin hugeuka nakuwa tamasha kubwa lililosheni sherehe, ada na desturi za aina tofauti kuanzia tangu majumbani, Misikitini hadi mabarabarani. Kila mahali huenea nyoyo zilijaa hali ya upendo na kusameheana, kuipokea Ibada na kufanya kila juhudi kwa ajili ya kujipatia thawabu na ujira mwema.

Ramadhani ina sehemu adhimu katika mioyo ya watu wa Benin ambapo hutumia muda mwingi kwa ajili ya Ibada na Itikafu Misikitini. Kwa kawaida, familia huwa hazipokei wageni majumbani mwao katika mwezi hu mtukufu kwa lengo lal kuepuka kupoteza wakati. Vilevile huepuka kupokea mialiko isiyokuwa ya lazima ya kuwatemdelea watu majmbani au kukutana na marafiki na majirani. Hakuna wakati wa kufanya kitu chochote zaidi ya kusoma Qur'an.

Lakini mara tu Idi inapotangazwa, furaha huenea nchini kote, na kugeuka kuwa tamasha la wazi tangu asubuhi hadi usiku, huku maadhi ya vikundi vikipita kupiga ngoma.

Kujitenga kwa ajili ya Ibada:

Kitu kinachovutia nchini Benin wakati wa mwezi huu mtukufu ni jinsi watu wanavyoipa umuhimu mkubwa Misikiti, amabpo hufanyiwa ukarabati na kupambwa nje na ndani. Jumuiya za hisani huzidisha sadaka ya Misahafu Misikitini kabl aya kuingia kwa mwezi wa Ramadhani. Baadhi ya watu huwadhamini wasomaji wa Qur'an na wanavyuoni khususan kutoka nchini Nigeria kwa ajili ya kuswalisha na kuendesha Dhikri na darsa za Tafsiri katika maeneo na vitongoji ambako hakuna Misikiti. 

Watu wazima na watoto, wake kwa waume, humiminika katika maeneo maalum ambayo hutayarishwa n akutandikwa kwa ajili ya Swala na vikao vya darsa za Kidini amabzo huanza baada ya Swala ya Adhuhuri na kuendelea mpaka wakati wa Swala ya Alasiri. Maeneo haya hupewa jina la "Tafsir". Baada ya Swala ya Alasiri watu huelekea majumbani kutayarisha Futari.

Kumi la mwisho la Ramadhani nchini Benin linazingatiw akuwa ni fursa adhimu ya kujikaurubisha kwa Allah سبحانه وتعالى, kwa kupiga Tahajjud na Itikafu, amabpo Misikiti hugeuka na kuwa minara inayotoa nuru kubwa. Baadhi ya Wakristo nao pia hufunga ili kuonesha mshikamano na Waislamu, nao Waislamu huvhukua jukumu la kuwapelekea Futari. Aidha moyo wa mshikamano na kuhurumiana huzidi kukua, ambapo Waislamu huzidisha kutoa sadaka kwa mafukara namasikini.

Kukhitisha Qur'an Katika Usiku Mmoja:

Miongoni mwa tofauti zinaoonekana wazi baina ya miezi ya kawaida na mwezi huu mtukufu ni kuwa harakati za kibiashara hupungua kutokana na watu kutumia muda mwingi kwa ajili ya Ibada.

Watu wengi huitumia fursa ya mwezi huu mtukufu kwa jili ya kutafuta maghfira. Kutokana na hali hiyo mioyo ya kusameheana hujaa baina ya watu. Matajiri na huchukua jukumu la vyakula, vinywaji na mavazi kwa jili ya maskini. Watu wenye uwezo hununua vitambaa kwa wingi na kuvigawa kwa maskini.

Usiku wa Laylatul Qadri unapewa umuhimu wa pekee nchini Benin, kiasi kwamba watu husoma Qur'ani nzima katika usiku huo. Baadhi ya familia huwaalika wanagfunzi kutoka madrasa za Qur'an katika maeneo maalum yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuswalia ikiwa katika eneo hilo hakuna Msikiti karibu. Kila mwanafunzi husoma Juzuu moja, na hujaribu kuimaliza Qur'an yote kabla ya Swala ya Asubuhi.

katika Usiku huu mtakatifu, watu hupena vyakula ili kupata baraka za usiku huu amabo wenyeji wa huko huuita "Usiku Mkuu"

Vyakula Vya Ramadhani:

Kama tulivyotangulia kudokeza kuwa Wabenin huacha shughuli zao kwa ajili ya kuzinyakua fadhila na baraka zote za mwaezi huu mtukufu. Mambo ya mijakulya haina umuhimu wowote katika mwzi wa Ramadhani. Kutokana hali hiyo hakuna mabadiliko ya vyakula, kwa maana nyengine, watu hawamaniki kwa kukosekana kemati, bali watu hula vyakula vya kawaid vilivyozoeleka.

Miongoni mwa vyakula maarufu nchini humo ni pamoja na supu ya njugu (karanga), uji wa Ilan ambao hutengenezwa kwa nafaka kama vile uwele, na mikate ya ndizi ijulikanayo kwa jina tali tali. Juisi nazo huwa haikosekani, khususan ya tangawizi mbichi.

Kwa kawaida watu huanza kufungua Swaumu kwa maji na tende amabazo mara nyingi huagizishwa kutoka nchi jirani ya Niger. Kisha watu huswali Magharib na baadaye kujipatia mlo rasmi. Watu hulala mara tu baada ya Swala ya Taraweh, na kiasi saa nane usiku akina mama huamka kutayarisha Daku.

Miongoni mwa vyakula maarufu pia, ni ugaliwa mahindi ambao hutayarishwa kwa njia za kijadi, siku kadhaa kabla ya Ramadhani na kuhifadhiwa kwa njia za kimila bila kuoza. Kila siku watu wakihitaji hukata pande, kupasha moto na kula. Pia hupatikana sambusa, lakini za huko badala ya nyama, hutiwa kunde au maharagwe ndani yake. Huwepo pia mikate ya kienyeji amabyo hutayarishwa kwa mchanganyiko wa nyunga za aina tofauti na kitoweo chake kwa kawaida huwa ni nyama ya kuku.

Itafaa kukumbusha kuwa Benin ina mchangavyiko wa makundi mengi ya kikabila na kijamii. Kwa hivyo vyakula na mavazi hutiofautiana kutoka eneo moja hadi jengine. Na kwa kawaida katika siku zenye umuhimu maalum kama vile harusi au Siku Kuu familia nzima huvaa sare moja. Ukiwaona tu utajua kuwa wale ni watu wa aila moja.

Hata hivyo kuna aina maarufu ya kitambaa ijulikanayo kwa jina la bomba amabyo kwa kawaida huvaliwa na watu wengi nyakati za kazi. Na ziko aina nyengine za vitambaa ambazo hutumika kwa ajili ya mavazi ya Siku Kuu na shughuli maalum.

Sherehe za Iddi:

Mara tu baada ya kutangazwa kuandama kwa mwezi, watu huonesha furaha yao ya kusherehekea Siku ya Iddi na kumshukuru Mola Mtukufu kwa kuwawezesha kukamilsha Faradhi ya Swaumu. Saa nne asubuhi familia nzima hutoka kuelekea kwenyey Swala ya Iddi.

Baada ya Swala, sherehe huenea kote, huku vikundi vya ngoma vikipita mitaani na kutumbuiza. Katika Mji Mkuu, vikundi hivyo huelekea katikati ya jiji ambako ndiko kwenye uwanja rasmi wa sherehe za Iddi. Sherehe hizo na furaha hudumu kwa siku nzima, na kuendelea kwa muda wote wa siku za Iddi.

Kinyume na siku za Ramadhani, kipindi cha Siku Kuu watu hutembeana na kubadlilishana zawadi. Familia hukutana kwa pamoja tangu babu hadi vilembwe. Na kwa mujibu wa mila za huko, mke wa mtoto wa mwisho ndiye mwenye jukumu la kutayarisha chakula kwa familia nzima. (Kwa hivyo ukiposwa na mwanamumue wa Benin kwanza muulize kama yeye ni mtoto wa mwisho au la).

Na kwa mujibu wa mila zao pia, watu wa mijini huwaalika jamaa zao kutoka vijijini na kujumuika nao pamoja wakati wa Iddi. Ikiwa mgeni kutoka shamba ni mgonjwa, basi itabidi wakae naye mpaka abese. Na ikiwa hali ya kimasiha ni ngumu huko anakotoka, basi itabidi wakae naye na kumhudumikia mpaka atakapo pata ajira mjini.

Na kwa mujibu wa mila za Benin, msimu wa Iddi watu huutumia kutangaza nia zao za kwenda kutekeleza Nguzo ya Tano ya Uislamu, Hijja.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako