If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, June 24, 2017

Ramadhani Ulimwenguni "BRAZIL''

Related image
Map Nchi ya Brazil (Picha via operationworld.org/braz)

Brazil inapatikana katika eneo la Amerika ya Kusini, au kwa jina jengine Latin America. Zamani Mji wake Mkuu ulikuwa ni Rio De Janeiro, lakini kutokana na sababu za kimkakati na kiuchumi, mnamo mwaka 1960 Mji Mkuu ukahamishiwa kuwa Brasilia. Hata hivyo jiji kubwa kabisa nchini humo ni Sao Paulo. 

Kwa hivyo watani wanasema Brazil ina Miji Mikuu mitatu: Brasilia, Mji Mkuu wa Kisiasa, Reo De Janeiro, Mji Mkuu wa Kitalii na Sao Paulo, Mji Mkuu wa kiuchumi.

Brazil inapakana na: French Guiana, Suriname, Guiyana,Venezuela, Columbia, Peru, Bolivia, Paraguay, Argentina na Uruguay. Kwa maana hiyo ni kusema kuwa inapakana na nchi zote za Amerika ya Kusini ispokuwa Chile na Ecuador. Lugha rasmi ya Brazil ni Kireno, na idadi ya watu wake inakadiriwa kiasi Milioni 206.

Linapotajwa jina la Brazil, jambo la mwanzo linalokuja akili mwa wengi ni Soka, kwani huko ndiko kwenye Kiti cha Enzi cha Mfalme wa Kabumbu, Pele. Hata hivyo Wabrazil nao wanatilia maanani maswala ya ibada, na Waislamu wako huko pia.

Idadi ya Waislamu nchini Brazil ni ndogo mno, kiasi kwamba katika machapisho mengi yanayozungumzia Dini tofauti na wafuasi wao nchini humo, Uislamu huingizwa kwenye orodha ya "Dini nyenginezo" ambayo inachukua kiasi 1.4%. Ndani ya hiyo 1.4% ndiyo umo Uislamu, kwa maana ni chini ya 1%. Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Sensa ya mwaka 2010, idadi ya Waislamu nchini Brazil ni 35,168, lakini jumuiya za Kiislamu nchini humo zinadai kuwa ni kiasi watu Milioni 1.5. Hta hivyo ni kiwango kidogo mno kulinganisha na idadi ya ujuml aya watu wote ambao ni kiasi 206.

Kuingia kwa Uislam Nchini Brazil:

Vyanzo vya Kihistoria vinaashiria kuwa Waislamu wa mwanzo kuingia nchini Brazil walikuwa ni Watumwa kutoka Afrika Magharibi. Kutokana na mazingira ya kiutumwa, Waislamu hao hawakuwa na uhuru wa kuabudu, na kwa hivyo walilazimika kutekeleza ibada zao kwa siri zikiwemo Swala na Swaumu ili kuepuka adhabu ya mijeledi pindi wakigundulika. Mnamo mwaka 1835 Waislamu hao walianzisha uasi na kufanya mapambano kwa ajili ya kujipatia uhuru wao katika jimbo la Bahia nchini humo. 


Ingawaje jaribio lao hilo halikufanikiwa na hivyo kupelekea kukandamizwa zaidi, hata hivyo vitabu vya historia vinalielezea tukio hilo kuwa ndilo jaribio kubwa kabisa la uasi wa Watumwa katika Mabara yote mawili ya Amerika.

Baada ya hapo yakafuatia makundi ya Wahamiaji kutoka nchi za Sham (Syria na Lebanon) na Uislamu kupata nguvu zaidi, huku wenyeji wakisilimu nakujiunga na Dini ya Allah.

Ramadhani Nchini Brazil:

Kwa vile Waislamu wa Brazil ni mchanganyiko wa Wahamiaji na wenyeji, Ramdhani nchini humo hujaa rangi tofauti za utamduni wa Kiislamu, huku kila mtu akibeba utamaduni wa nchi aliyotoka.

Simulizi za kihistoria zinaeleza kuwa Swala ya kwanza ya Tarawehe kuswaliwa kwa Jamaa nchini humo iliswalishwa na Sheikh Abdur Raman Al-Baghdady mnamo mwaka 1867 jijini Salvador katika Jimbo la Bahia. Na ili kuepesha udhia kwa Waislamu wa huko kwa wakati huo, aliswalisha Swala hiyo kwa Rakaa 10 tu.

Baada ya Wahamiaji kutoka nchi za Kiislamu kuzidi kumiminika, Waislamu wakaanza kujenga Misikiti na kuwapokea Maimamu na Mashekhe khususan katika mwezi wa Ramadhani ili kuupa heshima mwezi huu mtukufu. Hii ni kutokana na kuwa Ramadhani ni msimu maalum kwa Waislmau na ni fursa ya kuzidisha imani na kurejea kwa Mwenyezi Mungu.

Futari za Pamoja:

Misikiti na Taasisi nyingi za Kidini hufanya juhudi za kuandaa Futari za pamoja katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ingawaje baadhi yao hufanya kila mwishoni mwa Juma. Futari hizi za pamoja huwakutanisha Waislamu wote, maskini kwa matajiri, na ni fursa muhimu kwa wenye uwezo kutumia mali zao kwa ajili ya kuingiza furaha katika nyoyo za ndugu zao Waislamu. Futari hizi huwa pia ni tamasha la kiutamaduni ambapo kila mtu hupata nafasi ya kuleta vyakula vya utamduni wa asili aliyotoka, kama ambavyo ni nafasi ya kujuana baina ya Waislamu, na kuswali Swala ya Jamaa Msikitini.

Baadhi ya Jumuiya na Taasisi za hisani kutoka mataifa ya Kiislamu hutuma misaada kwa Misikiti au Jumuiya za Kiislamu nchini Brazil ili kufanikisha zoezi hili la futari za pamoja.

Kisomo Cha Qur'an:

Mwezi wa Ramadhani hutoa fursa ya aina yake kwa watu kukutana Misikitini na kuswali Swala ya Tarewehe. Baadhi ya Misikiti hujitahidi kukhitimisha Qur'an nzima, na mingine hukhitimisha katika kumi la mwisho la Mwezi huu mtukufu. Baadhi ya nchi za Kiislamu kama vile Misri kila mwaka hutuma Wasomaji wa Qur'an waliobobea ili kusaidia kukidhi mahitaji ya Maimamu kwa ajili ya kuswalisha Swala za Tarawehe, za Visimamo vya Usiku na kutoa darsa na mihadhara ya Kidini.

Usiku wa Laylatul Qadri:

Misikiti nchini Brazil hushindana katika kuweka ratiba bora kwa ajili ya Usiku huu wenye Cheo. Misikiti hujaa Waumini kwa vile familia nyingi hujihimu kwenda Misiktini na kukesha humo wakifuatana tangu mababu hadi vilembwe. Huswaliwa Swala ya Kisimamo cha Usiku, Kisomo cha Qur'an, Dua na baadaye watu hula daku kwa pamoja. Harakati hizi za ibada huendelea mpaka wakati wa Swala ya Alfajiri, na kwa watu wengi hii ni fursa ya kutubu kwa Mwenyezi Mungu.

Harakati za Kijamii:

Taasisi za Kiislamu nchini Brazil ziligundua umuhimu wa kuwa na mafungamano na jamii nyengi za nchi hiyo ili kuujulisha umma wa nchi hiyo juu ya sifa njema za Uislamu. Kutokana na hali hiyo zikaamua kuanzisha harakati za kijamii zinazolenga kuwasaidia watu maskini na wengineo. 

Harakati hizi huendeshwa na Umoja wa Kitaifa wa Kiislamu unaojumuisha taasisi na jumuiya nyingi za Kiislamu nchini humo ukiwa na Makao yake Makuu katika jiji la Sao Paulo. Kila mwishoni mwa wiki katika mwezi huu mtukufu, hufanyika kambi maalum kwa siku nzima katika moja ya vitongoji fakiri, ambapo hujumuisha matibabu ya bure ya aina zote pamoja na burudani kwa watoto.

Mbali na hayo, kambi hiyo hugawa vitabu na machapisho ya aina tofauti yanayokhusu Uislamu pamoja na kujibu maswali ya papo kwa papo ya watu wanaotaka kujua zaidi juu ya Uislamu. Hii ni njia bora kabisa ya kuendesha Da'awa, na kwa hivyo baadhi ya taasisi hizo zimeamua kuziendeleza shughuli hizo baada ya mwezi wa Ramadhani zikijumuisha mafunzo ya amali ili kuwawezesha watu kujipatia maarifa ya kujitafutia rizki zao.

Mashindano ya Utamaduni:

Misikiti na taasisi nyingi za Kidini nchini Brazil huandaa mashindano ya utamaduni na Kidini kwa vizazi vya Kiislamu nchini humo. Washindi kwenye mashindano hayo huaptiwa zawadi nzuri kama vile tiketi ya kwenda kufanya Umrah au kutembelea moja kati ya nchi za Kiislamu. Mashindano haya huamsha ari ya kujifunza na kujipatia maarifa mbali mbali mwiongozi mwa vizazi vya Kiislamu.

Tuzo kwa Wanazuoni:

Baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Taasisi za Kiislamu nchini humo huandaa sherehe maalum kwa ajili ya kutoa tuzo kwa Mashekhe na Wanazuoni wa ndani na wale waliokuja kutoka mataifa ya nje kwa jili ya kusaidia kuhuisha ibada katika mwezi huu mtukufu. Sherehe hii hutoa fursa kwa Wanazuoni hao kukutana ka kujuana, kubadilidhana uzoefu na kuendeleza moyo wa Upendo miongoni mwa Waislamu.

Vyakula Vya Ramadhani:

Kama tulivyodokeza hapo awali kuwa Uislamu nchini Brazil uliingia kupitia Watumwa na Wahamiaji kutoka nchi za Kiislamu, kwa hivyo, hakuna vyakula ambavyo tunaweza kusema kuwa ndivyo rasmi kwa ajili ya daku na Futari. 

Hata hivyo vyakula vingi maarufu katika mwezi huu mtukufu ni vile vyenye asili ya nchi za Sham kutokana na ushawishi wao mkubwa katika utamaduni wa Kiislamu nchini humo. Mbali na hivyo, kwa vizazi vipya vilivyozaliwa n akukulia nchini Brazil, hupendelea zaidi vyakula vya kijadi vya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako