If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, June 23, 2017

Ramadhani Ulimwenguni "CHAD''

Image result for CHAD MAP
Map Nchi ya Chad (Picha via operationworld.org/chad)

Location: Afrika ya Kati.

Mji Mkuu: N'djamena (Njamena)
Idadi ya watu: Milioni 14.

Idadi ya Waislamu: Zaidi ya 60% ya watu wake ni Waislamu,w engi wao wakiwa wa Madhehebu ya Sunni - Malik.

Kama zilivyo nchi nyingi za Kiafrika, Chad ilikuwa chini ya utawala wa kikoloni kwa miaka mingi. Ilijipatia uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960. Uislamu uliingia nchini humo katika karne ya kwanza, yaani mwaka 46 Hijriyah, sawa na mwaka 666 Miladiyyah. Ni mwanchama wa Umoja wa Nchi za Kiislamu Ulimwenguni. Kutokana na athari hizo za kihistoria, nchini Chad kuna lugha mbili rasmi; Kifaransa na Kiarabu.

Matayarisho ya Ramadhani nchini Chad:

Waislamu nchini Chad huupa umuhimu mkubwa mwezimtukufu wa Ramadhani. Wengi wao huanza maandalizi ya kufunga tangu mwezi wa Rajab na Shaaban, kwa maana baadhi ya watu hufunga miezi yote miwili ili Ramdhani inapowasili isiwe na uzito kwao.

Miongoni mwa desturi maarufu za maandalizi ya mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini humo ni ndoa, ambapo ndoa nyingi hufungwa siku chache qabla ya kuandama kwa mwezi ili mume awe na mke wa kukmtayarishia Futari nyumbani. Mara tu mwezi unapotangazwa kuandama rasmi, watu hujaa mitaani na kusherehekea kwa kupiga risasi hewani pamoja na fashifashi, kama ishara rasmi ya kumkaribisha mgeni huyu mtukufu.

Aidha, kufuatia kuandama kwa mwezi, Waislamu wa Chad husalimana na kutakiana msamaha. Kila mtu kuanzia na watu wa aila yake humwambia mwenziwe "tusameheane", ikiwa ni pamoja na kuombeana Dua na kutakiana kheri hapa Dunianai na kesho Akhera. Baada ya kupongezana watu wa aila moja, hutembelea ndugu, jamaa, marafiki na majirani na kuendelea kufanya hivyo.

Kwa upande mwengine, Waislamu nchini Chad hujiandaa na mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kukusanya vyakula vya kutosha kwa ajili ya Futari na Daku, na ikiwezekana kubadilisha ratiba na utaratibu wa kazi ili kupata nafasi na muda wa kutosha wa kufanya Ibada za mchana na usiku katika mwezi huu mtukufu.

Kwa upande wa watoto, wao hujenga misikiti ya udongo kwa ajili ya kuswalia na kusomea Qur'an. Pia nchini humo watoto huanza kuipewa mafunzo ya hukumu za Swaumu wakiwa na umrimdogo na kuanza kuzoeshwakufunga hatua kwa hatua.

Futari:

Wakati wa mwezi huu mtukufu, qabla ya jua kutua, milango ya nyumba za Waislamu huwachwa wazi ili kutoa nafasi kwa wapita njia kuingia na kujipatia Futari, khususan wale ambao wako njiani, kwa vile mpaka wakifika majumbani kwao muda wa kufutariutakuwa umewapita.

Mbali na wapita njia, mwezi huu wa Rahma, ni mwezi wa kuimarisha mshikamano wa kijamii, ambapo familia nyingi hufutari kwa pamoja na na kuwaalika wageni kujuika nao katika futari.
Vyakula maarufu vinavyopamba majamvi ya futari ni pamoja na: Supu au mchuzi wa nyama au kuku, ugali na uji mtamu ujulikanao kwa jina la madida. Siyo Ramadhani tu, bali hata katika siku za kawaida, madida haikosekani majumbani na hupendwa sana, si watoto si watu watu wazima.

Mwezi wa Ibada:

Waislamu nchini Chad huutumia vilivyo mwezi huu mtukufu kwa Dhikri, kuhudhuria kwenye darsa Misikitini, kusoma Qur'an na amali nyengine zinazopelekea katika njia ya kutafuta radhi za Mola wao. Nyakati za usiku hutumiwa kwa Taraweh na swala za Tahajjud.

Katika jumla ya kujitafutia fadhila za mwezi huu, Wachadi huwa na destrui ya kuwasaidia maskini na wasio jiweza, mayatima na kutayarisha futari kwa ajili ya maskini na wapita njia. majamvi ya futari hupatika kwa wingi pembezoni mwa barabara, mabustani na Misikitini.

Kumi la Mwisho:

Kumi la mwisho la Ramadhani linapoingia watu huzidisha Ibada. Waislamu wengi hujitahidi wasikose Tareweh, Tahajjud na Visimamo vya Usiku. Aidha hujumuika katika darsa za Tafsiri ya Qur'an, mawaidha, Visomo vya pamoja, ama Misikitini au katika madrasa.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako