If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, June 17, 2017

Ramadhani Ulimwenguni "CHINA''

Image result for CHINA
Location: Asia

Mji Mkuu: Beijing, lakini mji mkubwa kabisa ni Shanghai.

Idadi ya watu: Bilioni 1.337, ambayo ni sawa na robo ya watu wote Duniani. Idadi ya Waislamu ni kiasi milioni 20, wengi wao wakipatikana katika maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo. 

Msikiti mkubwa kabisa nchini humo unaitwa "Nyuu jii" na una umri wa zaidi ya miaka 1000. Adhana ya sauti huruhusiwa katika swala zote ispokuwa ya Alfajiri.

Kuandama kwa Mwezi: Imamu wa Msikiti Mkuu wa Nyuu Jii ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza mambo yote muhimu ya Kiislamu nchini China ikiwemo kuandama kwa mwezi wa Ramadhani ambayo Wachina wanaiita Chai yii.

Watoto wa kike hulazimishwa kuanza kufunga wakiwa na umri wa miaka 9, na wa kiume wakiwa na umri wa miaka 12. Wanaojitia ujuba na kupinga amri za wazazi wao za kufunga, hukiona cha mtema kuni. Na kama ilivyo desturi ya nchi nyingi za Kiislamu, Misikiti hufurika zaidi wakati wa mwezi huu Mtukufu.

Maandalizi ya Ramadhani: Kwa kawaida Waislamu wa China hujiandaa mapema kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramdhani ikiwa ni pamoja na kulundika vyakula vya lazima kwa jili ya Futari na Daku pamoja na kukalimisha shughuli zote za lazima ili wapate muda wa kutosha wa kufanya Ibada katika mwezi huu wa Rahma na Baraka. Pia Maimamu na Masheikh huongeza juhudi za kueneza Da'awa na mawaidha khususa yanayohusiana na kutoa mwamko juu ya Ramdhani ili kuwaandaa watu kiroho na Kiimani katika kuukabili mwezi mtukufu.

Futari: Mara tu baada ya Adhana ya Magharibi, Waislamu nchini China hukimbilia kupata Sunna ya kuwahi kufungua Swaumu. Awamu hii ya kwanza kwa kawaida huanza kwa chai ya kijani (green tea) au chai ya kawaida ambayo hutiwa sukari nyingi, kisha kufuatiwa na tikiti maji. Bila tikiti maji, futari haijatimia nchini China.

Baada ya hapo watu huelekea kuswali swala ya Magharibi na baadaye kuanza rasmi awamu ya pili ya futari. Awamu hii ndiyo hujumisha mlo mkuu amabo chakula muhimu huwa ni wali na vikorobwezo vyengine vitokanavyo na mchele. Pia hupatikana vyakula vyengine vitamu, mboga mboga na matunda kama vile doriani, maembe na mengineyo amabyo hatunayo katika eneo la Afrika Mashariki. Nyama si kawaida kwao, kwa vile Wachina wanapenda kuepuka vyakula vyenye mafuta mengi na kolestrol. Juisi na sharbati za aina tofauti pia huwepo pembeni.

Watu hula Futari Miskitini ambako kila mtu hupeleka chakula alichojaaliwa, au majumbani ambako ukoo mzima hukusanyika kula Futari ya pamoja. Meza ya kulilia huwa na umbo la duara, na inaweza kuzunguka ili kila mtu aweze kupata chakula kilichopo mezani bila kujiumiza musuli kwa kupemba vyakula vilivyo mbali naye.

Sadaka: Utoaji wa Sadaka hushamiri pia nchini China katika mwezi huu mtukufu. Kwa kawaida watu wenye uwezo hujitolea kufutarisha watu ama misikitini, majumbani au kutoa sadaka kwa njia nyenginezo ikiwemo fedha taslim kwa ajili ya kutafuta radhi za Mola wao.

Ramadhani ni kwa watu wote: Waislamu wa China wana desturi ya kulishana, kwa maana kwamba kila Mwislamu huwapelekea vyakula na zawadi nyengine ndugu jamaa na majirani hata wasiokuwa Waislamu. Kutokana na hali hiyo, baadhi ya Wachina wasiokuwa Waislamu hushirikiana na majirani zao Waislamu katika utamaduni huu wa kubadilishana vyakula na zawadi, na hata kula nao futari pamoja. Kwa ujumla hushirikiana nao katika ada nyingi za Ramadhani bila kuwabughudhi huku wakitunza heshima ya mwezi huu Mtukufu kiasi kwamba wengine hufikia hadi kufunga.

Ramdhani ni mwezi wa Ibada: Baada ya Futari Waislamu huelekea Misikitini kwa ajili ya Swala ya Isha, Tarawehe na Tahajjud. Kwa kawaida watu wa huko huswali Taraweh kwa rakaa 20. Aidha huweko darasa na mihadhara mingi ya kidini. Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha nchini Misri hutuma Masheikh kila mwaka kwa jili ya kuwasaidia Masheikh wa huko katika kutoa mihadhara na kusoma na kusomesha Qur'an. Usije ukawachezea watoto wa Kichina kwa kusoma Qur'an, watakubwaga chini.

Mandhari ya Ujumla ya Ramadhani: Waislamu wa China huupa heshima inayostahiki mwezi huu mtukufu, na hujizuia na mambo yote yaliyoharamishwa na mengineyo ya anasa. Kuvuta sigara mchana ni fedheha kubwa kwa Mwislamu, na akionekana mtu hadhari, basi jamii humsuta, na atajuta kwa nini akafanya kosa hilo. Katika maeneo mengi, khususan vijijini, wasiokuwa Waislamu pia husaidia kulinda heshima ya mwezi huu ili kutowabughudhi jirani zao.

Hakuna mapambo rasmi ya Ramadhani kama ilivyo katika baadhi ya nchi za Kiislmu ispokuwa Misikitini.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako