If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, June 24, 2017

Ramadhani Ulimwenguni "ERITREA''

Image result for Eritrea
Map Nchi ya Eritrea (Picha via operationworld.org)

Eritrea inapatikana Mashariki mwa Afrika, katika eneo lijulikanalo kama Pembe ya Afrika (Horn of Africa). Inapakana na Ethiopia, Sudan, Djibuti na Bahari ya Sham.
Mji wake Mkuu ni Asmara.

Idadi ya watu wake ni takriban milioni 5.

Kuna takwimu za kutatanisha kukhusu idadi ya Waislamu nchini Eritrea, lakini takwimu zote zinazunguka kwenye 50% ya watu wote.

Eritrea ilikuwa ni sehemu ya Ehtiopia mpaka pale ilipojitangazia uhuru wake mwaka 1991 kufuatia miaka 30 ya mapambano ya harakati za uhuru yaliyoongozwa na wapiganaji wa Eritrean People's Liberation Front (Jeshi la Ukombozi wa Watu wa Eritrea).

Eritrea iko kwenye eneo la kimkakati katika Prmbe ya Afrika, ikichungulia kwenye Bahari ya Sham. Kwa hivyo, kujiengua kwake kuliiwacha Ethiopia kuwa nchi isiyo na bandari. Aidha hatua hiyo ya Eritrea ilitia ukokmo wa Himaya ya Uhabeshi (The Abyssinian Empire) iliyoanza tangu karne za kale ikisambaa kutoka Pembe ya Afrika hadi Yemen na kuselelea kwa miaka na dahari.

Kuupokea Mwezi wa Ramadhani:

Kabla ya kuandama kwa mwezi wa Ramadhani, watu waliokhasimiana nchini Eritrea husameheana na kusafiana nia. Watu pia hushughulika na kuipamba Misikiti na kuifanyia ukarabati nje na ndani. Baada ya Ofisi ya Mufti kutangaza rasmi kuandama kwa mwezi, kila Mwislamu huelekea katika nyumba ya Mkuu wa Ukoo wao, ambako ukoo mzima hukutana, kusalimiana, kupongezana kwa kuingia kwa mwezi mtukufu, kusameheana kwa wale waliokoseana ha hatimaye kula daku pamoja.
Kwa ujumla khazina ya utamaduni wa Kiislamu hufunguliwa, ambapo Misiskiti hujaa Waumini, na vikao vya darsa, dhikri na kuhifadhi Qur'an huanza. Mshikamano wa kijamii huongezeka na kupata nguvu miongoni mwa ndugu, jamaa na majirani, na watoto hujaa furaha nyoyoni katika kipindi chote cha mwezi mtukufu.

Mandhari ya Ujumla na Ada zake:

Waeritrea huanza maandalizi ya Ramadhani kwa kutayarisha aina mbali mbali za vyakula, wiki mbili au zaidi kabla ya kuandama kwa mwezi. Miongoni mwa vichopozi maarufu ambavyo hutayarishwa khususan katika maeneo ya milimani ni achari ambayo hutengenezwa kwa mchanganyiko wa viungo tofauti na kuchapuzwa kwa pilipili kichaa. Ni achari kali ambayo kama hukiuanza kuizoea tangu utotoni itakutoa machozi.

Nyakati za usiku katika mwezi huu mtukufu huweko vikao maalum, khaswa khaswa kwa akina mama na wasichana, ambapo huwa wanakutana katika nyumba ya mmoja wao kila usiku kwa mzungumko baada ya Swala ya Tarawehe. Katika vikao hivyo, akina mama hujishughulisha na kazi za mikono khususan ushonaji wa kofia kwa ajli ya wanaume, ufumaji wa vitambaa na mapambo mengine kwa ajili ya Iddi. Aidha watu wamezowea kuandaa Futari na kuzipeleka Miskitini, kwa familia za watu masikini au wazee wasioweza kujitayarishia Futari zao.

Kuonekana Kwa Mwezi:

Ofisi ya Mufti wa Eritrea ndiyo inayosimamia rasmi zoezi la kuutafuta mwezi mwandamo katika maeneo ya nyanda za juu ya nchi hiyo. Watu hwenda kwenye maeneo ya milimani kuangalia mwezi. Wanaouona hutakiwa kutuma taarifa kwa kituo cha Polisi kilicho karibu nao. Na kama mwezi haukuonekana, basi kwa kawaida Waeritrea hufuata mwezi mwandamo wa Saudi Arabia.

Maandalizi ya Futari:

Katika mwezi huu mtukufu wa Ramdahni, akina mama hutayarisha Futari ambayo kwa kawaida hujumuisha supu amabyo hutayarishwa baada ya Swala ya Adhuhuri au Alasiri. Supu hiyo hutayarishwa kwa nyama, ngano iliyotwangwa na viungo mbali mbali. Huchemshwa kwa moto mdogo. Karibu na jua kutua hupaswa moto na kuongezwa siagi. Kwa aghlabu supu hiyo huliwa na sambusa.

Katika jamvi la Futari pia hupatikana samaki wa kupaka, tende, juisi za matunda, kaimati, uji na vikorobwezo vyengine. Kwa ujumla vyakula vya futari nchini humo havitofautiani sana na vile vya maeneo ya Afrika Mashariki.

Vigoma vya Daku:

Kama ilivyo katika nchi nyingi za Kiislamu, vigoma vya Daku huwa vinapatikana nchini Eritrea. Huko vimebandikwa jina la "Daku yako Mfungaji". Hii inatokana na maneno ya mwanzoni mwa nyimbo maarufu ya kuamshia Daku ambayo inasema: "Daku yako Ewe Mfungaji, na Neema ni zako wewe Mola wa daima, Allah ndiye Mola wako, na Muhammad ndiye Mtume wako. Amka Ewe mwenye kulala, jipatie Daku yako Ewe Mfungaji".

Kwa kawaida vigoma vya Daku nchini humo kupigwa na vikundi vya vijana ambao huzunguka katika meneo yao maalum. Nyumba wanayomalizia kumsha, hujumuika na wenyeji wa nyumba hiyo na kula nao Daku pamoja. Kila familia huomba nyumba yao iwe kituo cha mwisho cha waamshaji ili waweze kuwakaribisha kula nao Daku na kujipatia fadhila za Mola wao katika mwezi huu wa kheri na Baraka.

Halkadhalika Waislamu nchini Eritrea hushereheka pale mtoto anapokhitimu kiwango fulani cha Qur'an. Anapohifadhi Juzuu moja hufanyiwa sherehe ndogo. Na anapohifadhi Msafahafu wote, hapo hufanyiwa sherehe ya aina yake ambayo huambatana na kuchinjwa mnyama na kualikwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wanafunzi wanaosoma Madrasa moja.

Chakula maarufu cha Daku ni wali kwa nyama, tambi na makaroni.

Utamaduni wa Kahawa:

Baada ya Futari, Waeritrea wana utamaduni wa kahawa ijulikanayo kwa jina la "Jabanah". Kahawa hukaangwa na kutwangwa, kuchanganywa na viuongo kama vile tangawizi na hiliki na kuchemshwa kwa mkaa ndani ya chombo maalum kijulikanacho kwa jina Jabanah, na hii ndiyo asili ya jina la kahawa hiyo. Jabanah ni mtungi mdogo kiasi ya birika kilichotengenezwa kwa udongo.

Kwa kawaida Jabanah hunywewa na mikate ya kijadi iitwayo Hambasha iliytengenezwa kwa ustadi mkubwa. Vilevile sukari huwepo pembeni kwa wanaopenda, na hunywewa ikiambatana na kuchomwa udi. ukikosekana udi Jabanah haijakamilika. Hunywewa kwa mzunguko wa awamu tatu. 

Huanza kwa wamu ya kwanza ambapo kila mtu hupata kikombe kimoja, na awamu hii huitwa "utangulizi". Kisha chungu huwekwa tena kwenye makaa na baada ya kuchemka kuanza awamu ya pili ijulikanayo kama "baraka", na kendelea kama hivvyo mpaka wanapochoka huku udi ukiendele kufukuta.

Darsa za Kidini:

Mwezi wa Ramdahni nchini Eritrea una ladha yake, ambapo watu hujizuia na maaswi, mpaka walevi huacha kunywa kwa kuupa heshima mwezi huu mtukufu, na wengine huwa ndio mwanzo wa kuacha kabisa bisa tabia hiyo mbaya. Misikiti hujaa Waumini wake kwa waume, na kila Msikiti huteua Mashekhe ambao hutoa darsa za Kidini. Darsa hizo ambazo huambatana na Dhikri na Nyiradi huanza baada ya Swala za Adhuhuri na Alasiri.

Aidha, katika baadhi ya maeneo khususan Mji Mkuu Asmara, watu hupeleka vyakula Misikitini katika siku za Ijumaa na Jumatatu ambapo husomwa Maulid. Na katika kumi la mwisho la Ramadhani, au hata kabla ya hapo, watu hupeleka vyakula Misikitini kama Sadka kwa ajili ya ndugu na jamaa zao waliotangulia mbele ya haki.

Iddi:

Siku ya Iddi ni siku ya Furaha kwa Waislamu kote ulimwenguni , na hivyo nchini Eritrea. Iddi hupokelewa kwa furaha na watu huvalia mapavazi mapya na mazuri amabyo kwa wanaume mengine huwa yametengenezwa kwa mikono na wanawake kama tulivyotangukia kutaja hapo awali. 

Mbali na kanzu nyeupe na kofia ambayo nchni Eritrea inaitwa hivyo hivyo kwa wanaume pia vazi la kijadi huambatana na kizibao. Wanawake huvaa mvazi yao ya kijadi ikiwemo ile inayofanana na kanga pamoja na vito vyengine vya thamani, bila kusahau hina.

Hii ni siku ya furaha zaidi kwa watoto ambao hupita majumbani kwa ndugu na jamaa zao na kujipatia zawadi za Iddi.

Msikiti wa Maswahaba:

Kama tulivyodokeza, Eritrea ilikuwa ni sehemu ya Ethipia. Na katika toleo letu lililopita tuligusia kuwa Maswahaba wa Mtume صلى الله عليه وسلم walifika huko katika kile kijulikanacho kama Hijira ya Kwanza. Walisafiri kupitia Bahari ya Sham na kufikia katika mji wenye Bandari Kuu katika nchi ya Eritrea ya leo. 

Huko kuna Msikiti ambao unasadikiwa kuasisiwa na Maswahaba hao. Katika miaka ya mwanzo ya Uislamu watu walikuwa wakiswali kuelekea kwenye Qibla cha Baytul Maqdas, jijini Jerussalem. Kwa hivyo mpaka leo Msikiti huo haukubadilishwa Qibla chake ili kuhifadhi hadhi yake ya Kihistoria, na watu humiminika kwa wingi kuswali swala za Iddi ili kujipatia Braka za Msikiti huo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako