If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, June 21, 2017

Ramadhani Ulimwenguni "ETHIOPIA''

Image result for ETHIOPIA
Map Nchi ya  Ethiopia (Picha via operationworld.org)

Ethiopia, ambayo pia katika historia inajulikana kwa jina Abyssinia, inapatikana Mashariki mwa Afrika katika eneo lijulikanalo kama Pembe ya Afrika.'

Mji wake Mkuu ni Adis Ababa, na ndiko kwenye Makao Makuu ya kudumu ya Umoja wa Afrika.
Idadi ya watu wake ni kiasi Milioni 100, Waislamu wakichukua 34%.

Lugha rasmi ni Amharic (Kiamhari), na inaandikwa kwa herufi zake yenyewe badala ya zile za Kizungu au Kiarabu kama ilivyo katika nchi nyingi za Kiafrika.

Ethiopia ni moja kati ya nchi zenye ustaarabu wa kale ulimwenguni. Kinyume na nchi nyingi Barani Afrika, nchi hiyo haikuwahi kutawaliwa na Wakoloni. Ilikuwa ni katika Waasisi wa Umoja wa Mataifa mwaka 1945 wakati mataifa ya Kiafrika yakiwa chini ya tawala za Kikoloni, na pia ni moja ya mataifa waanzilishi wa Umoja wa Afrika.

Uislamu uliwasili nchini Ethiopia kabla ya mji wa Madina. Kwa maana hii ni kusema kuwa ni ardhi ya pili ulimwenguni kufikiwa na Uislamu baada ya mji wa Makka. Waislamu waliingia nchini Ethiopia iliyokuwa ikijulikana kama Uhabeshi katika kile kijulikanacho katika historia ya Kiislamu kama Hijra ya Kwanza.

Ni vizuri kukumbusha kuwa, Uislamu ulipata upinzani mkubwa katika miaka ya mwanzo katika mji wa Makka, na Waislamu walikabiliwa na unyanyasaji, mateso na ukandamizaji wa kila aina kutoka kwa Makafiri. Kutokana na hali hiyo, kikundi cha Waislamu kikaondoka mji wa Makka na kuelekea Uhabeshi ili kusalimisha maisha yao na kutafuta uhuru wa kuabudu. Hii ikawa ndiyo Hijra ya Kwanza, na walipofika huko walipokelewa na kukirimiwa vizuri na Mfalme wa Uhabeshi.

Hijra ya pili ni pale Mtume محمد صلى الله عليه وسلم alipohama kutoka Makka na kuhamia Madina na kuasisi Dola ya Kiislamu

Ramadhani Nchini Ethiopia:


Kama ilivyo katika nchi nyingi ulimwenguni, Waislamu wa Ethiopia huupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa furaha na bashasha huku wakiomba dua kwa Mola Mlezi wapate kheri hapa duniani na kesho Akhera. 

Kwa muda wa miongo kadhaa, Ethiopia imekuwa ikikabiliwa na vipindi vya ukame mkali. Kwa hivyo, miongoni mwa Dua maarufu kwa Waislamu wa nchi hiyo ni kumwomba الله سبحانه وتعالى awaondoshee balaa hili kwa baraka za mwezi huu mtukufu.

Kutokana na hali ngumu za kimaisha nchini Ethiopia, harakati za Ramadhani na maandalizi yake hutofautiana na nchi nyengine. Lakini hali hiyo ngumu ya kiuchumi haijawafanya Waethipia kuacha ada na desturi nzuri za mwezi huu mtukufu tangu enzi na dahari.

Harakati Zilizojaa Hamasa:

Mandahari za kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Ethiopia zinaonekana wazi masokoni. Familia za Kiislamu huzidisha harakati zao masokoni kwa ajili ya kujinunulia mahitaji ya lazima ya mwezi huumtukufu kwa mujibu wa uwezo wao. 

Hujitahidi kuupa umuhimu mkubwa mwezi huu kwa lengo la kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa amali njema na kutoa sadaka. Hii ni kutokana na kuwa wanahisi kuwa wana wajibu mkubwa walioachiwa na mababu zao ambao walifuzu kwa kuwapokea Maswahaba wa Mtume صلى الله عليه وسلم waliokuwa wakikimbia mateso ya Makafiri wa Makka zaidi ya karne 14 zilizopita. Mababu zao waliwapokea Maswahaba hao kwa ukarimu mkubwa.

Kuenea Kwa Utamaduni wa Kiislam:

Kila mwaka, Wanazuoni na Walinganiaji kutoka mijini hadi vijijini huzidisha harakati zao katika mwezi huu mtukufu kuliko nyakati nyengine. Misikiti husafishwa, kutiwa rangi, maandishi na mapambo ya kuta nje na ndani hufanyiwa ukarabati na ikiwezekana kutiwa mazulia mapya. 

Mabadiliko haya hufanyika zaidi katika misikitki ya mijini kuliko ya vijijini. Ama katika maeneo ya vijijini, harakati za utamaduni wa Kiislamju huchangamka zaidi nchini Ethiopia kwa kupitia Madrasa na Vyuo Vya Kiislam.

Ibada za Usiku:

Wafanyakazi wa Kiislamu nchini Ethiopia huchukua likizo zao wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa vile hupendelea kuwemo Misikitini katika hali ya utulivu na unyenyekevu. 

Huutumia mwezi huu kwa kufuata maelekezo ya Bwana Mtume صلى الله عليه وسلم aliposema: "Mbora wenu ni yule mwenye kujifundisha Qur'an na kuifundisha". Mbali na Kisomo cha Qur'an, nyakati za usiku hupendelea kukaa Misikitini kwa kupiga Nyiradi na Dhikri kwa unyenyekevu.

Swala ya Tarawehe:

Swala ya Tarawehe huswaliwa kwa wingi nchini Ethiopia, khususan katika maeneo ya vijijini, na huendelea mpaka usiku wa manane katika siku 20 za mwanzo za Ramadhani. Ama katika kumi la mwisho, ibada hiyo huendelea mpaka wakati wa Swala ya Alfajiri kwa vile huwa inaambatana na Swala ya Tahajjud. Wakulima hutupa majembe yao ya kawaida na kubeba majembe ya ibada kuelekea kwenye mashamba ya Ramadhani Misikitini.

Nyakati za Swala za Tarawehe na Ijumaa, Waumini hufurika katika Msikti mkubwa kabisa nchini humo ujulikanao kwa jina la "Masjid Anwar" ambao unapatikana katika Mji Mkuu Adis Ababa. Msikiti huo huwa hautoshi kubeba maelfu wa Waumini wanaomiminika, na hivyo barabara zote kuu hufungwa ili kutoa nafasi kwa Waislamu kutekeleza ibada zao huku wakipewa ulinzi wa Polisi.

Mama N'tilie:

Katika baadhi ya maeneo, akina mama na hata baadhi ya wasichana wadogo, hukaa mabarabarani takriban saa moja au mbili kabla ya Adhana ya Magharib na kuuza futari. Aghlabu vyakula wanavyouza huwa ni falafel, sambusa na uji wa shairi. Chapati huwa pia hazikosekani ambazo wenyeji wa huko huziita "Njara", na hiki ndicho chakula maarufu kabisa nchini Ethiopia. Wafungaji wengi huwategemea Mama N'tilie kwa ajili ya futari, khususan wale ambao kutokana na sbabu moja au nyengine hushindwa kutayarisha futari majumbani mwao.

Futari:

Waislamu wa Ethiopia hupendelea sana vyakula vya protini na uwanga. Kutokana hali hiyo, bei za nyama maziwa na bidhaa nyengine zitokanazo na maziwa hupanda katika mwezi huu mtukufu. Miongoni mwa bidhaa ambazo hukumbwa na mfumko wa bei ni pamoja na chakileti, tende na mirungi (miraa) ambayo imekuwa ni moja kati ya vitu vya lazima katika futari.

Mirungi:

Baadhi ya Waislamu nchini Ethiopia hupendelea kutafuna majani ya mirungi kwa imani potofu kuwa huwasaidia wakati wa ibada na kuwakurubisha kwa Allah. Mirungi huanza kuliwa mara tu baada ya Futari ili kuwasaidia watu katika Dhikri, ibada na Swala ya Tarawehe, kiasi kwamba baadhi ya Misikiti huchelewesha Swala za Isha na Tarawehe kwa ajli ya kutoa muda wa kutosha kwa watu kujipatia miraa au kama inavyojulikanavyo kwa jina jengine Gat, kwa vile inaaminika kuwa ni kichangamsho kizuri kinachowasaidia watu kuwa macho na kuweza kutekeleza ibada za Tarawehe na Tahajjud.

Kula mirungi ni katika ada mbaya zilizozoeleka nchini Ethiopia katika mwezi huu mtukufu ambao ndio msimu mkubwa wa mauzo ya bidhaa hiyo ambayo tafiti nyingi zimethitisha kuwa ina madhara makubwa kwa afya ya binadamu, kiasi baadhi ya Wanazuoni kufikia kutoa fatwa za kuiharamisha.

Biasha ya Misuaki:

Mbali na ada hiyo mbaya ya kula mirungi, hata hivyo Waislamu nchini Ethiopia wanazo mila nzuri za kuhuisha Sunna katika mwezi huu mtukufu. Miongoni mwa Sunna hizo ni ile iliyogogotezwa ya kupiga msuaki.

Biashara ya misuaki ya miti hushamiri zaidi katika mwezi huu kwa vile watu hupendelea kupiga misuaki mara kwa mara ili kupunguza harufu mbaya ya kinywa wakati wa Swaumu. Biashara hii huwajumuisha zaidi wajasiriamali vijana wa kike kwa kiume ambao huendesha harakati za mauzo katika masoko makubwa, mitaani, vituo vya usafiri na maeneo ya karibu na Misikiti.

Katika mwezi huu wa fadhila, inakadiriwa kuwa wajasiriamali hao hujiingizia kipato cha hadi Dala 5 kwa siku, ambacho ni zaidi ya kipato cha wafanyakazi wa viwandani nchini humo.

Wahenga walisema "Mgeni awiya mwenyeji apone". Kwa hivyo mgeni mtukufu wa Ramadhani anapoawiya nchini Ethiopia wanaopona siyo Waislamu peke yao, bali hata Wakristo. Kwani wajasiriamali wa Dini hiyo nao hujitupa katika biashara ya misuaki ambayo msimu wake mkuu ni mwezi huu mtukufu na kufaidika na baraka zake.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako