If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, June 21, 2017

Ramadhani Ulimwenguni "JORDAN''

Image result for jordan country map
Map ya Nchi ya Jordan ( Picha na orldatlas.com)

Location: Jordan inapatikana katika Bara la Asia katika eneo maarufu lijulikanalo kama Mashariki ya Kati. Imepakana na Saudi Arabia, Israel, Syria na Irak. Mji Mkuu ni Amman (عمان)

Idadi ya watu: Kiasi milioni 9, na zaidi ya 95% ni Waislamu. Kati yao 92% ni Waislamu wa Madhehebu ya Sunni na 1% ni wa Madhehebu ya Shia na Sufi.

Kuandama kwa mwezi: Kwa kawaida Mufti wa nchi hiyo ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza rasmi kuandama kwa mwezi na hivyo watu kuanza kufunga.

Vyakula vya Ramadhani: Kwa kawaida watu hufungua kwa Sunna ya tende, kwenda kuswali Magharib na baadaye kula futari rasmi.

Majamvi ya futari hupambwa kwa vyakula vya aina tofauti. Mansaf ni moja kati ya vyakula maarufu nchini Jordan na mara nyingi hupatika katika majamvi ya futari. Chakula hiki ni sawa na pilau iliyotengenezwa kwa mchele, nyama ya kondoo, maziwa ya mgando (yogurt), viungo vya aina mbalimbali, matunda na kutandikwa kwenye mikate ya Kiarabu (pita bread).

Vyengine vinavyopatikana ni pamoja na nyama za aina tofauti, hummus, mbogamboga, wali wa kawaida na achari.

Vinywaji maarufu ni juisi za aina tofauti: Bwana Suhaib ni mwenyeji wa jiji la Zarqa lililoko katikati ya Jordan, anasema "Mimi kama hakuna juisi ya ukwaju, basi kwangu mimi futari haijatimia"
Aidha, huwepo vitu vitamu (desserts) kama vile baklava, kunafah, halva na qatayef ambazo hutengenezwa maskhsusi kwa ajili ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 


Matunda pia hayakosekani kwa mujibu wa msimu khususan tikiti maji ambalo ni muhimu kwa wafungaji kwa vile hutoa virutubishi vya kutosha na kukata kiu.

Mahema ya Futari: Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, baadhi ya watu hujenga mahema maalum kwa ajili ya Futari. Mahema hayo hupatikana tangu mijini mpaka maeneo ya vijijini, na hujengwa na mtu mmoja mmoja, familia au mashirika ya biashara. Mtu yoyote yule hukaribishwa kujiunga katika hema lolote na "kujisikia". 

Mahema yanayojengwa na mashirika ya biashara au watu matajiri ni sawa na zile "Meza za Mwenyezi Mungu" tulizozielezea nchini Misri, ambapo watu hufutarisha kwa ajili ya kutafuta radhi za Mola wao.

Baada ya futari: Watu huelekea kwenye Swala ya Taraweh, na kwa watoto ambao hawakufuatana na wazazi wao kwenda kwenye Ibada hiyo muhimu, hujishughulisha na michezo mbalimbali ikiwemo fashifashi. Hii ni biashara kubwa katika msimu huu, na mitaa yote hujaa moshi wa fashifashi.

Mihadhara ya Kidini hushamiri katika mwezi huu Mtukufu, kama ambavyo huweko harakati nyengine za kijamii ikiwemo michezo ya aina tofauti.

Sadaka: Sadaka hutolewa kwa wingi katika mwezi Mukufu wa Ramadhan, mara nyingi baada ya swala ya Taraweh. Hutolewa kwa viwango tofauti ama na Misikiti au waja wema waliopewa uwezo na Mola wao. Hii huwasaidia sana maskini kwa ajilii ya matumizi ya Iddi na baadaye, khususan ikizingatiwa kuwa wanaweza kula bure kila siku katika Mahema ya futari.

Daku: Kwa kawaida daku kujumuisha Sehemu iliyobaki ya Mansaf, wali, nyama na matunda. Kwa vile Jordan ni moja kati ya wazalishaji wakubwa wa Zaytuni duniani, matunda hayo huwa hayakosekani kwenye daku, ama matunda yenyewe au vitu vyengine vitokanavyo na zao hilo kama vile mafuta ya kupikia, viungo na mengineyo. Maziwa ya mgando pia huwepo pembeni pamoja na matunda: Anasema Bwana Bahaaud Din, mwenyeji wa Amman: "Mimi sijisikii kula daku kama sijapata nyama ya kutosha"

Vigoma vya daku: Kama ilivyokawaida kwa nchi nyingi za Kiislamu, waamshaji wa kula daku hawakosekani. Kwa nchini Jordan, waamshaji hao huwa ni mtu mmoja mmoja, na badala ya vigoma vidogovidogo tulivyovizowea kwetu, nchini Jordan waamshaji hubeba magoma mazito mfano wa beni na hutembea mitaani kwa maeneo maalum. 

Pamoja na kuwa muamshaji huwa ni mtu mmoaj, lakini kwa kawaida hupata wasaidizi ambao huwa ni watoto wanaotafuta njia tofauti za kupitisha usiku wa Ramadhani huku wakisubiri Daku iwe tayari nyumbani.

Maudhui kuu ya nyimbo zao huwa ni kuwausia watu waamke kula daku, kwa vile ni Sunna na muna baraka ndani yake, pia kuwausia watu kumcha Mwenyezi Mungu na kudumisha Swaumu na Ibada nyengine.

Baada ya Mfungo wa ramadhani kumalizika, waamshaji hupita katika maeneo yao na kukusanya ujira wao ambao huwa ama fedha taslim, hidaya au vyote.

Wakati wa Mchana: Kwa kawaida migahawa yote hufungwa nchini Jordan wakati wa mchana katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ispokuwa katika maeneo maalum yenye leseni za Kitalii kama vile mahoteli makubwa. 

Ni marufuku kwa watu kula mchana hadharani.

Mandhari: Mandhari ya miji na vijiji hupambwa kwa mapambo maalum kwa ajili ya mwezi huu mtukufu zikiwemo taa maarufu zijulikanazo kama fawaniis. 

Mapambo haya hupatikana takriban kila nyumba, na hivyo kuleta faida kubwa kwa wafanyabiashara. Maeneo ya Kitalii nayo pia hupambwa kwa mapambo ya umeme yenye kuakisi mandhari ya wmezi Mtukufu.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako