If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, June 20, 2017

Ramadhani Ulimwenguni "MISRI''

Image result for egypt map
Map ya egypt (Picha via maps-africa)

Location: Afrika ya Kaskazini

Idadi ya wakaazi wake: Zaidi ya Milioni 91, na zaidi ya 90% kati yao ni Waislamu.

Kuthibiti kuandama kwa mwezi: Kwa kuonekana mwezi, au kutimia siku 30 za Shaaban, na Mufti wa nchi hiyo hutangaza rasmi kuanza kwa Ramadhani.

Wakati wa kuanza kufunga na kufutari: Kwa kawaida hupigwa mzinga ambao huashiria kuwa muda wa kunga umefika, kwa hivyo kama una kitu mdomoni ukiteme. Pia mzinga huo hulia tena wakati wa kufungua unapowadia.

Mzinga huu hupigwa Mji Mkuu wa chi hiyo, Cairo, lakini sauti yake hurushwa hewani moja kwa moja na vyombo vya khabari.

Vyakula vya Ramadhani:

Kama ambavyo chakula ni sehemu muhimu ya utamaduni wa watu, utamaduni huu hutofautiana baina ya nchi na nchi, eneo hadi eneo, na vivyo hivyo wakati wa Ramadhani.

Wakati ambapo katima maeneo mengi ya Afrika Mashariki, uji ni sehemu muhimu katika futari, nchini Misri hali ni tofauti. Kwao, vinywaji maarufu wakati wa futari ni chai au vinyaji vyengine baridi kama vile "Yansun", "karkadee" na vyenginevyo.

Ama kwa upande wa vyakula vikuu, mikate haikosekani, khusuan ile ambayo kwa jina la kienyeji inaitwa: "Eish". Hii ni aina ya mikate inayojulikana kimataifa kama "pita bread". Unapoumuka huwa kama mfuko, na unapoukata unapata sehemu mbili zilizowazi na kuingiza vyakula vyengine ndani yake, kama kitoweo, mbogamboga na vyenginevyo. Mbali na mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mikate hii ndicho chakula muhimu kwa Wamisri katika siku za kawaida, naserikali hujitahidi kuhakikisha kuwa unga wake hauadimiki na unapatikana kwa bei nafuu.


Katika kudumisha Sunna ya Bwana Mtume صلى الله عليه وسلم tende pia huwa hazikosekani katika jamvi la futari. Maduka husheheni aina tofauti ya tende. Ni vizuri kukujulisha mpenzi msomaji kuwa zao la tende linapitia hatua mbalimbali kama vile nazi. 

Ziko za makoroma, zilizoiva kwa wastani, zilizoiva kupindukia (za madebe) na mpaka kavu (kama mbata). Kwa hivyo aina zote hizi hupatikana madukani wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramdhani.

Pembezoni mwa hizo hupatikana wali uliochangwanya na tambi, kuku au nyama ya aina yoyote ile, bila kusahau vitu vitamu.

مائدة الرحمن "Maaidatur-Rahman" wingi wake ni: موائد الرحمن (Mawaaidur-Rahman)

Tunaweza kuitafsiri kama "Meza ya Mwenyezi Mungu". Hizi ni sehemu ambazo watu huandaa Futari, na sehemu nyengine haa Daku kwa ajili ya watu wasiojiweza au waliopatwa na dharura kama vile wasafiri na wengineo. Sehemu hizi hupatikana katika mitaa mingi na kwa viwangio tofauti. 

Watani wanasema ziko za "nyota tano", ambazo huandaliwa na watu wenye uwezo mkubwa kifedha. Kwa kawaida watu kama hawa kutiliana mikataba na mahoteli makubwa makubwa kwa ajili ya kuwaandalia Futari na Daku katika maeneo ambayo wateja huyachagua. Ama majumbani wanakoishi, Misikitini, majumba ya mayatima, maeneo ya wazi na kwengineko.

Vyombo Vya Khabri wakti wa Ramdhani:

Kwa kawaida vipindi vya redio na Televisheni hubadilika wakati wa mwezi huu Mtukufu, na vipindi vya kidini hupewa nafasi zaidi. Kwa upande wa burudani, vyombo hivyo hutayarisha michezo maalum kwa ajili ya mwezi hu احياء ليلى رمضان (Ihyaa'u layaali Ramadhan).

Mchana ni wakati wa kufunga na kutafuta rizki, ama wakati wa usiku Waislamu nchini Misri huutumia wakti wa usiku kwa njia na mifumo tofauti. Iliyo maarufu kabisa ni Ibada za Swala, kuhudhuria mawaidha na mihadhara ya Kidini.

Hata hivyo sehemu ya kijamii nayo hupewa nafasi yake pia. Nyakati za usiku huweko michezo ya aina mbali mbali ikiwemo ya kuigiza na burudani nyengine za kienyeji.

Hata Mpira wa miguu ambao ndio mchezo maarufu kabisa nchini humo, hupewa nafasi yake. Kunakuweko na ligi ndogo ndogo za kandanda tangu kwenye vilabu vikubwa mpaka vichochoroni. Ligi zenyewe zaweza kuwa za idadi ya kawaida ya wachezaji au watu sita-sita kwa kila timu.

Vigoma vya Daku: " مسحرات (Musahhiraat)

Vimepewa jina hilo kwa vile huwaamsha watu kula daku (سحور) "suhuur".

Waamshaji hao huwa ama vikundi vya watu hata mtu mmoja mmoja. Na kila mtu au kikundi huwa na 'himaya' yake maalum ambako mipaka yake haiwezi kuingiliwa. Siku ya Idi inapofika kila mtu au kikundi hupita katika maeneo yao na kukusanya ujira wa kazi yao ya mwezi mzima. 

Ujira huo huo huweza kuwa fedha taslimu, zawadi au vyote viwili. na hakuna kiwango maalum cha utoaji, kila mtu na uwezo wake, almradi ni kuonesha shukrani kwa kazi nzuri ya mwezi mzima.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako