If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, June 19, 2017

Ramadhani Ulimwenguni "NIGER''


Mji Mkuu Niamey

Idadi ya watu: kiasi milioni 19

Inapatikana katika eneo la Afrika Magharibi, na sehemu yake kubwa iko katika jangwa la Sahara. Idadi ya Waislamu: Zaidi ya 97% ya watu wake ni Waislamu. 95% kati yao wakiwa wa Madhehebu ya Sunni - Malik, na 5% ni Shia.

Uislamu uliingia nchini Niger tangu miaka ya mwanzo ya Uislamu, yaani mwaka 46 Hijriyah, sawa na 666 Miladiyah. Uislamu ulijikita na kuota mizizi huko kwa miaka mingi, na nchi hiyo ni mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Ulimwenguni (OIC).

Baadaye zikaja enzi za ukoloni wa Ulaya Barani Afrika, na Niger ikaangukia chini ya Ukoloni wa Kifansa. Pamoja na kujipatia Uhuru wake tangu mwaka 1960, athari za ukoloni bado zinaendelea kuonekana wazi, na moja kati yao ni Lugha. 

Licha ya kuwa idadi kubwa ya watu wake ni Waislamu, lakini Kifansa bado ndiyo lugha rasmi ya nchi hiyo. Lugha ya Kihausa inazungumzwa kwa wingi nchini Niger pamoja na lugha nyengine za kikabila. Pamoja na athari hizo za ksiasa na kijamaii, hata hivyo ukoloni haukuweza kuzima nuru ya Kiislamu nchini Niger, na Uislamu unaendelea kushika nafasi kubwa katika mwenendo wa ujumla wa kimaisha nchini humo.

Mapokezi ya Ramadhani Nchini Niger:

Wa-Niger wana mfumo wa pekee wa kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Wao tangu kati kati ya mwezi wa Shaaban, vikundi maalum hutoka na vigoma na mizumari kila siku kuwakumbusha watu kuwa mwezi mtukufu unakaribia.

Mwezi 29 Shaaban, makundi ya watu hutoka kwenda kuangalia mwezi, na mara baada ya kutangazwa kuonekana kwake, Msafara rasmi hutoka na kupiga matari mitaani kutangaza kuwasili kwa Mgeni huyu mtukufu.

Mila nyengine zilizozoeleka za kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kwa wanaume kutuma zawadi nono kwa familia za wachumba wao. Kwa upande wa wanaume waliooa, nao hupeleka zawadi za vyakula bora ukweni mara tu baada ya kuandama kwa mwezi. Msafara wa kwenda ukweni husindikizwa na watoto na vijana ambao huwa wanapiga tari.

Futari:

Kama ilivyo kwa Waislamu wengi ulimwenguni, Futari ndio mlo mkuu wa kila siku katika mwezi mtukufu wa Ramadhnai nchini Niger. Kwa kawaida kwao futari hujumuisha supu iliyopikwa kwa mbogamboga na mchanganyiko wa viuongo tofauti. Hii ni kwa ajili ya kufungua kinywa na tumbo na kuchapuza hamu ya kula.

Aidha hupatikana makaroni na mayai, bila kuusahau ugali ambao katika nchi za Afrika Magharibi huitwa fufu. Fufu ndicho chakula muhimu kabisa katika futari nchini Niger. Baada ya hapo watu huelekea misikitini kwa ajili ya darsa na miadhara amabyo hupatika usiku mchana katika mwezi mzima wa Ramadhani.

Vyombo vya khabari navyo hubadilisha ratiba zao ambapo vipindi vya kidini huchukua nafasi kubwa zaidi. Na katika kumi la mwisho la Ramadhani, Wafungaji hupiga Itikafu Misikitini na kuhuisha Sunna ya Swala za Kisimamo cha usiku (Qiyamul Layl)

Laylatul Qadri:

Usiku wa Laylatul - Qadri unapewa umuhimu wa aina yake nchini Niger, kiasi kwamba inatambuliwa na Serikali kama Siku Kuu rasmi. Rais wa nchi hiyo, Waziri Mkuu na Maqadhi huswali Laylatul - Qadri katika Msikiti Mkuu ulioko jijini Niamey.

Vigoma Vya Daku:

Kinyume na ilivyozoeleka katika nchi nyingi Duniani, nchini Niger vigoma vya daku hupita mara mbili. Mara ya kwanza hupita kuwaamsha watu kula Daku, na mara ya pili kupita kuwakumbusha watu kuwa muda wa kuanza kufunga umekaribia, na kwa hivyo watu wapate tone la mwisho la maji.

Siku ya Iddi, kama ilivyo desturi, wapiga vigoma ambavyo kwa kawaida huwa vya mfumo wa tari, hupita mitaani kuchukua zawadi zao. Watu huwapa zawadi nono wapiga vigoma kama kuwashukuru kwa juhudi zao za mwezi mzima.

Kuhifadhi Qur'an:

Swala la kuhifadhi Qur'an nchini Niger linapewa kipaumbele, amabpo wazazi wengi hufanya juhudi za kuwahifadhisha watoto wao Qur'an Takatifu katika mwezi wa Ramadhani. Watoto hupelekwa katika vituo maalum vya kuhifadhisha Qur'an vijulikanavyo kwa jina la Man'dara. Wanafunzi huishi huko kwa muda wote wa mafunzo yao ambayo kwa kawaida huanza mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhani.

Walimu au Mashekhe wanaoendesha vituo hivyo hawalipwi ujira kwa pesa taslim. Bali wanafunzi husaidia katika shughuli za kilimo na matengenezo na matunzo ya vituo hivyo. Baada ya mwanafunzi kumaliza kuhifadhi Qur'an, familia yake humuandalia sherehe kubwa. Ikiwa kahitimu katika mwezi wa Ramadhani, basi huandaliwa Futari maalum kwa ajili yake, huku wakialikwa wanfunzi wenzake na mwalimu wake kujumuika nye katika hafla hii ya akifakhari.

Familia hujisikia fakhari mtoto wao anapokamilisha kuhifadhi Qur'an, na katika usiku wa sherehe hiyo adhimu, huchinjwa mnyama kwa heshima ya mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako