If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, June 10, 2017

Ramadhani Ulimwenguni ''Tajikistan''

Image result for tajikistan
Location: Asia ya Kati. Inapakana na: Afghanistan, China, Kyrgyzstan na Uzbekistan.

Mji Mkuu: Dushambe.

Idadi ya watu: Zaidi ya milioni 8

Idadi ya Waislamu: Zaidi ya 95% ni Waislamu, wengi wao wakiwa wa Madhehebu ya Sunni - Hanafi. Madhehebu ya Shia yanachukua 5% ya Waislamu wote.

Tajikistan ni moja kati ya mataifa ya Kiislamu yenye historia ndefu. Uislamu uliingia huko tangu karne za mwanzo na ni moja kati ya vituo muhimu vya utamaduni wa Kiislamu. Wanazuoni wengi Mashuhuri ama walipita, kuishi au kusoma katika taifa hilo, kama vile Mwanachuoni maarufu wa Hadith, Imam Al-Bukhari.

Kwa muda wa zaidi ya miongo 7 (miaka 70), Tajikistan ilikuwa chini ya Umoja wa Kisovieti. Na kama ijulikanavyo Sovieti ilikuwa ikiendeshwa chini ya siasa za Kikomunisti ambazo zilikuwa haziruhusu uhuru wa kuabudu kwa dini zote. Kwa maana hiyo, Uislamu ulikuwa chini ya ukandamizaji mkubwa.

Hata hivyo Waislamu waliendelea kusimama kidete na kushikama na Dini yao, na wakati mataifa yaliyokuwa katika Umoja wa Kisovieti uliongozwa na Urusi yalipoanza kudai uhuru wao, viongozi wa Kiislamu katika Jamhuri ya Tajikistan walikuwa msitari wa mbele kabisa katika harakati hizo.

Baada ya kusambaratika kwa Umoja wa Kisovieti na kujipatia tena uhuru wao mwaka 1991, wananchi wa Tajikistan walirejesha haiba ya taifa lao kama jamii ya Kiislamu.

Maanadalizi ya Ramadhani:

Kuja kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni sawa na ukumbusho kwa Waislamu wa Tajikstan juu ya utukufu wa historia yao na mchango mkubwa uliotolewa na Wanazuini wao katika Dini. Kwa hivyo hufurahi kwa kuandama kwa mwezi na hujitayarisha kwa ajili ya kuutumia vyema mwezi huu mtukufu kwa ajili ya Ibada, na kuzidi kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu.


Waislamu wa Tajikstan, wanaungalia mwezi huu mtukufu kama fursa ya kuimarisha utamaduni wa Kidini. Na mara tu unapotangazwa kuandama, hukunja mikono ya mashati yao kama ishara ya furaha ya kuwasili na kumkaribisha mgeni huyu mtukufu mwenye fadhila na baraka, na kujitayarisha kuzitumia vyema fadhila zake.

Ufunguzi wa Misiskiti:

Siku chache kabla ya kuandama kwa mwezi wa Ramadhani, Waislamu wa Tajikistan hujitahidi kufungua Misikiti mipya ili ipate baraka za mwezi huu mtuku, na maeneo ya misikiti hutandikwa majamvi kwa ajili ya vyakula kwa wapita njia na wengineo wenye kuhitaji.

Kuzembea Swaumu ni mwiko:

Jambo la kufurahisha ni kwamba uzembe katika Ibada ya Swaumu ni mwiko, kiasi kwamba Waislamu nchini humo huwalazimisha watoto wao kufunga wakiwa na umri wa miaka 9. Na mtoto asiyefunga, basi marafiki zake humwambia kuwa si Mwislamu au si raia wa nchi hiyo, na kwa hivyo atafute nchi yake aende.

Katika mwezi huu mtukufu, watoto huchukua mifuko ya plastiki na kutembea nyumba hadi nyumba kwa ajili ya kukusanya zawadi. Wanapofika mlangoni huimba: "Umefika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Ewe mwenye nyumba, tunakutakia Ramadhani yenye baraka, basi toka utupatie zawadi yetu".

Kuongezeka kwa harakatiza kibiashara:

Harakati za maisha nchini humo hazisimami kwa sababu ya mwezi wa Ramadhani, bali mwezi huu huzidisha harakati na kuongeza ladha maalum ya maisha na biashara. Kwa mfano, katika Mji Mkuu Dushambe, harakti za maisha huchangamka zaidi na jiji hujaa watu wakiwemo wageni wanaozuru mji huo na wafanyabiashara. Biashara za mitaani huongezeka, mara utamkuta huyu katandika jamvi, yule kaweka meza na namwengine kajenga kibanda wakiuza bidhaa za vyakula na nyenginezo. Huyu utamuona anauza mikate ya Kitajiki aliyoitengeneza kwenye tanuri lake la nyumbani, yule anauza vyakula vitamu maalum kwa ajili ya Ramadhani na vyakula vyengine vya kienyeji, na mwengie anauza Tasbihi, Miswala, kalenda za Ramadhani na mengineyo.

Harakati za Misikitini:

Baraza la Taifa la Maswala ya Kidini likishirikiana na Vituo na Vyuo vya Kiislamu, huzidisha harakati zao katika mwezi huu mtukufu. Kwa vile tayari watu wamo katika hali ya Imani ya juu kutokana na Swaumu, basi taasisi hizo huitumia fursa hii kwa kutayarisha vipindi maalum vya kitamaduni na kifikra vyenye lengo la kutoa mwelekeo mzuri na mwamko wa Kiiislamu.

Mshikamao baina ya matajiri na masikini:

Miongoni mwa mambo yanayovutia nchini Tajikistan katika mwezi huu mtukufu, ni mshikamano baina ya matajiri na masikini, ambapo wale waliojaaliwa kipato na Mola wao huchukua dhamana ya kuwafutarisha waisojiweza. Watu hao wema huwaalika maskini kila siku ili kuftari nao pamoja majumbani mwao baada ya Swala ya Magharibi, ikiwa ni katika kutafuta fadhila za Mola wao.

Vyakula vya Futari:

Upishi ni sanaa inayopewa kipaumbele nchini Tajikistan. Kwa hivyo mwezi mtukufu wa Ramadhani unapoingia kila nyumba hupambwa kwa aina mbalimbali za vyakula vulivyotayarishwa kwa ufundi mkubwa.

Miongoni mwa viungo muhimu vinavyokamilisha mlo wa Futari ni pamoja na chai ya maziwa ambayo wenyeji wa huko huiita "Shirchai"( sijui kwa kwetu ndiyo chai ya shira hiyo?). Aidha hupatikana chakula kitamu kijulikanacho kwa jina la "Nishalda au Nishollo", kutegemea na eneo mtu anakotoka. Chakula hiki hutengenezwa kwa sukari, mayai na mmea aina ya licorice. Juise na matunda makavu pia havikosekani kwenye jamvi la futari.

Supu pia huwepo kwenye futari, na ni sehemu muhimu. Supu maarufu hutengenezwa kwa vichinyango vidogo vidogo vya nyama, tungule, vitunguu, mbatata na viazi vya carrot. Halkadhalika huwepo pilau ya kienyeji ijulikanayo kwa jina "Plov". Hutengenezwa kwa: mchele, nyama, carrot, na vitunguu thaumu vizima bila kusagwa.

Swala ya Taraweh:

Waislamu hujihimu sana kuswali Swala tano kwa Jamaa. Na nyakati za Swala za Isha na Tarawehe Misikiti hufurika Waumini. Baadhi ya Misikiti hukhitimisha Qur'an katika kipindi cha siku tatu katika Swala ya Tarawehe, mingine hukamilisha katika muda wa wiki moja, na iko inayochukua mwezi mzima kama ilivyozoeleka katika misikiti mingi.

Kumi la Mwisho la Ramadhani:

Kumi la mwisho la Ramadhani linapoingia waumini nchini Tajikistan hujitahidi kuhakikisha kuwa wanalitumia vizuri kwa Ibada. Misikiti mikubwa na midogo pamoja na maeneo ya kuswalia Swala ya Ijumaa yote hujaa Waumini wanaokesha humo hadi asubuhi wakiitafuta Laylatul Qadri kwa Swala, Dua na kusoma Qur'an. Wenyewe Watajik wanaziita siku hizi "Siku za Kisimamo", na kila mmoja hapendi zimpite. Na hii wanaizingatia kuwa ni njia bora kabisa ya kuuaga mwezi huuMtukufu.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako