If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, June 13, 2017

Ramadhani Ulimwenguni ''URUSI''

Related image

Baada ya kuzizungumzia Jamhuri tatu zilizokuwa chini ya Umoja wa Kisovieti, leo tunalizungumzia "kubwa lao", Urusi.

Urusi ndiyo nchi kubwa kabisa kieneo Ulimwenguni. Iko katika eneo lijulikanalo kam "Euro-Asia", kwa vile eneo lake kubwa liko Ulaya ya Mashariki, na sehemu iliyobakia iko Barani Asia. Kwa kawaida katika majukwaa ya kimataifa Urusi hushiriki kama nchi ya Ulaya.

Ina watu zaidi ya Milioni 144, Mji wake Mkuu ni Moscow.

Idadi ya Waislam ni kiasi millioni 20, amabyo ni sawa na takriban 11% ya watu wote.

Kinyume na nchi nyingi za Ulaya, Waislamu wa Urusi hawatokani na kizazi cha Wahamaiaji, kama vile ilivyo Ujerumanai ambako Waislamu wengi wanatoka Uturuki, Bara Arabu na kwengineko. Bali Waislamu wa Urusi ni wenyeji wa asili, na ni sehemu muhimu katika jamii ya nchi yao.

Idadi kubwa ya Waislamu nchini Urusi inapatikana katika maeneo ya Volga-Ural na Kaskazini mwa Caucas. Maeneo mengine ikiwemo miji mikubwa kama vile Moscow au Saint-Petersburg, pia yana idadi kubwa ya Waislamu.

Urusi ina mfumo wa Shirikisho, ikijulikaan Kimataifa kama "Russian Federation" Kwa hivyo, Jamhuri ambazo zinatambulika kama ni za Kiislam, tukimaanisha kuwa idadi kubwa ya wakaazi wake ni Waislamu ni Jamhuri za Bashkortostan na Tatarstan zinazopatikana katika eneo la Volga-Urals , na Jamhuri za Ingushetia, Dagestan, Kabardino-Balkaria na Karachay-Cherkessia zilizoko Kaskazini mwa eneo la Caucas.

Kuingia kwa Uislamu nchini Urusi:

Uislamu una mizizi mirefu nchini Urusi. Uliingia nchini humo tangu katikati ya karne ya 7 ukianzia katika Jamhuri ya Dagestan na kuendelea kusambaa katika Maeneo ya Kaskazini mwa Caucas. Ilipofika mwaka 21 Hijriyah (641 Miladiyyah) Uislamu ulifika katika maeneo ya Kusini mwa Caucas, na hii ni baada ya kulidhibiti eneo la Ufursi, lijaukanalo leo hii kama Iran na maeneo ya karibu.

Kama tulivyoiita "kubwa lao", mpenzi  msomaji itafaa kukumbusha kuwa Urusi ndiyo iiliyokuwa kinara wa Umoja wa Kisovieti. Na baadhi ya wachambuzi wanadiriki kusema kuwa nchi zote zilizounda Umoja huo zilikuwa chini ya Utawala wa Kimabavu wa Kikomunisti ulioongozwa na Urusi. Kutokana na hali hiyo, na kama tulivyodokeza katika makala zilizotangulia, mfumo wa Kikomunisti ulikuwa hauruhusu uhuru wa kuabudu, na hali hiyo iliuathiri Uislamu na Waislamu wa urusi pia.

Mwenyezi Mungu anasema:
يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ" " (8) سورة الصف

Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.

Kwa hali hiyo, Waislamu nchini Urusi waliendelea kushikama na Dini yao na ktekeleza Ibada zao kama vile Swaumu japo kisirisiri na kwa kadiri walivyoweza. Baada ya kusambaratika kwa Umoja wa Sovieti mwaka 1991, Uislamu ulihuika tena nchini humo, na hata kufikia baadhi ya Jamhuri zenye Waislamu wengi kama vile Chechniya kujitangazia uhuru wao, ingawa majaribio hayo hayakufanikiwa, lakini wakapata kiasi kikubwa cha mamlaka ya ndani.

Baada ya maelezo hayo, sasa tuingalie Radhani nchini Urusi.

Waislamu nchini humo hujitayarisha kuipokea Ramadhani kwa furaha na bashasha wakiizingatia kuwa ni fursa adhimu ya kuimarisha Imani zao na utamaduni wa Dini yao. Misikiti nchini humo amabyo inakaribia 8,000 hujaa Waumini kwa ajili ya Ibada ya Swala na Dua. Jiji la Moscow lina misikiti mikubwa mitano, amabayo hujaa kwa Ibada, na adhana katika Misikiti hiyo huadhiniwa kwa sauti kila wakati wa Swala. Kwa maana nyengine ni kusema kuwa inaswaliwa Swala Tano kwa Jamaa.

Masiha katika mwezi wa Ramadhani:

Mara tu baada ya kuandama kwa mwezi, maisha ya Waislamu nchini Urusi hubadilika ili kwenda sambamba na hadhi na heshima ya mwezi huu mtukufu. Huhakikisha kuwa hawakosi Swala za Jamaa Misikiti, pamoja na Ibada nyengine maalum za mwezi huu. Hata hivyo maisha na mandhari ya Ramadhani hutofautiana kutoka eneo moja hadi jengine, ikizingatiwa kuwa Urusi ni nchi kubwa yenye mazingira tofauti ya kijiografia na kijamii. Itafaa kudokeza kuwa Warusi Wanafunga masaa mengi, kuanzia 19 hadi 22 katika baadhi ya maeneo. Kwa hivyo Warusi ni vidume kwa Ibada, usije ukawaona kuwa ni Mizungu.

Pamoja na mazingira hayo, bado Warusi wanaizingatia Ramadhani kuwa ni nafasi ya pekee yakujikurubisha kwa Mola wao na kuzidi kuongeza imani, khususan kwa wale ambao huwa tunawaita "Waislamu jina". Hawa nao kwa baraka za mwezi mtukufu hurejea katika mwenendo sahihi, na hii husaidia pia kupelekea wasiokuwa Waislamu kuingia katika Dini.

Meza za Futari:

Waislamu wa Urusi wanaishi katika jamii isiyokuwa ya Kiislamu, kwa vile wao ni wachache. Na kutokana na ukubwa wa nchi yao, kuna makundi ya kijamii na kikabila yenye mila ada na desturi tofauti, ambazo Waislamu hujikuta wamekwama humo wakiwa kama wanajamii hizo. Kwa hivyo katika baadhi ya miji ya nchi hiyo, huandaliwa futari za pamoja ambazo hufadhiliwa na Watenda Kheri wa kienyeji kwa kushirikiana na taasisi na Jumuiya za Kiislamu za Kimataifa.

Ama kwa wale wanaofutari majumbani mwao, hali haiko tofauti sana. Kwani kila ukoo hufutari pamoja, ikiwa ni pamoja na kuwaalika majirani. Baba huswalisha familia yake wakati wa swala ya Magharibi, na hujitahidi kuwapatia futari nzuri wageni waalikwa ambayo aghlabu hujumuisha wali, nyama, supu, vitu vitamu vilivyotengenezwa kwa njia za kienyeji na vyenginevyo.

Katika sehemu za vijijini, Waislamu huwaalika Waumini wa Msikiti baada ya Swala ya Maghrib kuja kufutari majumbani kwao. Kwakufanya hivyo, wenyeji wa n yumba na majirani walioalikwa hufaidika kwa visomo vya Qur'an, Dua mawaidha na darsa zinazotolewa na Maimamu wanaohudhuria mialiko yao au wanafunzi wao. Hii huleta athari nzuri kwa wageni waalikwa na kusaidia wale Waislamu jina kuwajibika na mafunzo sahihi ya Dini yao.

Hema la Ramadhani:

Tukio amablo husubiriwa kwa hamu kubwa kila mwaka ni ufunguzi wa Hema la Ramadhani katika mji Mkuu wa nchi hiyo Moscow. hema hili hujengwa kila mwaka katika eneo lililo karibu na Msikiti Mkubwa katika kitongoji cha Kihistoria jijini Moscow. Kila siku huandaliwa futari katika hema hilo ambalo lina uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 600. Kila mtu hukaribishwa hapo kujipatia mlo wa bure, bila kujali Dini rangi, kabila jinsia au lolote. Almradi uende na tumbo lako tu.

Hema hilo huandaliwa na Baraza la Mamufti wa Urusi, hata hivyo hukaribisha makundi mengine ya utamaduni na sanaa kushiriki katika tamasha hilo la kila mwaka. Mbali na Baraza la Mamufti, wanaoshiriki ktika udhamini na maandalizi ni pamoja na Mamlaka ya jiji la Moscow na taasisi nyengine za Kidini. Kuna vikundi vya Dini, Utamaduni na Sanaa kutoka maeneo mbali mbali ya Urusi huja kushiriki katika tamasha hilo.

Kwa ufupi hili ni huwa ni tamasha au jukwaa la Dini zote. Mbali na kupatikana futari ya bure, Waislamu hupata faida ya kuwavutia wasiokuwa Waislamu na kuwapiga Da'wa. Kwa hivyo hii inakuwa ni frsa ya pekee ya kuutangaza Uislamu.

Swala ya Tarawehe:

Kama ilivyo katika nchi nyengine, nchini Urusi Swla ya Tarawehe kupewa umuhimu wake, na Misikiti hujaa Waumini wanaziwinda fadhila za mwezi huu mtukufu, kuzidi kujikaribisha kwa Mola wao na kuzidiha Imani zao. Kwa kawaida Misikiti mingi hukhitimisha Qur'an japo mara moja kwa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako