If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, June 15, 2017

Ramadhani Ulimwenguni "UZBEKISTAN''

Image result for UZBEKISTAN

Karibu tena mpenzi msomaji katika mfulululizo wetu wa makala zetu......

Katika toleo liliopita tulikuwa katikati ya Bara la Asia, na leo bado tunabakia huko huko. Tunavuka mpaka kutoka Tajikistan na kuingia Uzbekistan:

Mji Mkuu: Tashkent.
Idadi ya watu: Zaidi ya milioni 30.
Lugha rasmi: Kiuzbeki.

Idadi ya Waislamu: Zaidi ya 95%, wengi wao wakiwa wa Madhehebu ya Sunni - Hanafi.

Mpenzi msomaji, huenda hii ikawa ni mara ya kwanza kulisikia jina la Uzbekistan. Lakini ukweli ni kwamba, jina hili ni maarufu kwako. Kitabu swahihi kuliko vyote duniani ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Qur'an Takatifu, kinachofuatia kwa usahihi ni Swahih al- Bukahari (صحيح البخارى).

Mwanachuoni maarufu Muhammad Ismail al-Bukhari aliyeandika kitabu hicho alizaliwa nchini Uzbekistan. Kama ilivyo nchi jirani ya Tajikistan, Uzbekistan ilikuwa moja kati ya Jamhuri zilizounda Umoja wa Kisovieti chini ya Utawala wa Urusi. Chini ya utawala huo wa Kikomunisti ambao ulikuwa hautoi uhuru wa kuabudu, Uislamu ulikuwa chini ya ukandamizaji mkubwa. Baadhi ya Misikiti, Madrasa na majengo mengine ya Kidini yaligeuzwa kuwa majengo ya kijeshi, maskuli, au majengo mengine ya serikali. Licha ya kuwa Kiuzbek ndiyo Lugha rasmi, lakini bado Kirusi kinazungumzwa kwa wingi, kwani enzi za Kisovieti ndiyo iliyokuwa Lugha rasmi.

Waislamu walikuwa hawaruhusiwi kufunga, na kwa hivyo walikuwa wakifunga kwa siri, na wale waliogundulika walipata adhabu. Hata hivyo Waislamu waliendelea kushikamana na Imani yao thabiti, na baada ya nchi hiyo kujipatia tena Uhuru wake mwaka 1991 kufuatia kusambaratika kwa Umoja wa Kisovieti, uhuru wa kuabudu ulirejea tena, Misikiti, na vituo vyengine vya Kiislamu vikaanza kurejesha haiba na hadhi yake ya kihistoria. Na mwaka 1996 ilijiunga rasmi na Umoja wa Nchi za Kiislamu.

Kwa maelezo hayo mpenzi msikilizaji, inafaa kukudokeza kuwa Uislamu uliingia nchini Uzbekistan katika mwaka wa 30 Hijria wakati wa Ukhalifa wa Sayyidna Othman Bin Affan رضي الله عنه, na hii ni baada ya kufunguliwa kwa nchi ya Ufursi (Iran ya leo). Na moja kati ya nakala za asili za Msahafu wa Sayyidna Othman RA inapatikana huko.

Samarkand ndio uliokuwa Mji Mkuu wa taifa hilo na kituo muhimu cha harakati za kiutamaduni na Kiislamu. Katika jiji hilo walipita na kusihi Wanazuoni wengi wakiwemo Iman al-Bukhari, Imam Tirmidhy, Ibnu Siina na wengineo wengi. Pia kunapatikana Msikiti mkubwa na Chuo kinachotoa wasomi wa Kidini vikibeba jina la Imam al-Bukhari.Warusi walipoivamia nchi hiyo na kuiingiza katika Shirikisho la Kisovieti, Mji Mkuu ukahamishiwa na kuwa Tashkent mpaka leo hii.

Baada ya mukhtasari huo, sasa tuangalie Ramadhani nchini Uzbekistan.
Kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani:

Wananchi wa Uzbekistan huupokea mwezi mtukufu kwa hali ya furaha. Licha ya kuwa Wauzbeki wengi ni Waislamu, lakini pia wako wasiokuwa Waislamu. Hata hivyo wote wanashikamana na kujivunia uzalendo wao. Kutokana na hali hiyo, wale wasiokuwa Waislmau nao pia hujisikia furaha mwezi unapoandama na hushirikiana na ndugu zao Waislamu katika kusherehekea kuwasili kwa mgeni huyu mtukufu.

Kiwango cha joto:

Katika nchi hiyo, kiwango cha joto huwa kikubwa kias ikufikia nyuzi 40 baaadhii ya nyakati na hivyo kupelekea uchofu mkubwa kwa Wafungaji. Hata hivyo, hilo haliwazuii Wauzbeki kutekeleza Ibada ya Swaumu, bali huendelea kufunga kwa furaha na hata kuwahamasisha watoto wao kufunga.
Kufurika kwa Misikiti:

Ramadhani inapofika huwakumbusha Waislamu wa Uzbekistan juu ya utukufu wa historia yao na utamaduni wao kama tulivyogusia hapo awali. Huchangamka na kuitikia Ulinganio wa mababu zao Wanazuoni wakubwa walitoa mchango mkubwa katika Uislamu. Misikiti hujaa pomoni! Barabara zote na maeneo waliyoishi, kusomea au kupita Wanazuoni wao na kutoa Elimu za fani tofauti hupambwa kwa mapambo ya aina yake.

Mgeni mmoja kutoka Bara Arabu anaelezea mshangao wake kuwa, katika mwezi huu mtukufu, Waislamu wa huko huupamba kwa visomo vizuri vya Qu'an Takatifu kuliko Waarabu wenyewe, na hii ni kuthibitisha na kutamba kuwa nchi yao ni kitovu cha kihistoria cha Elimu ya Kiislamu na utamaduni wake.

Futari ya Pamoja:

Moja kati ya mambo yanayovutia nchini humo ni mfumo wa Futari. Waislamu wa Uzbekistani wana desturi ya kuwaalika ndugu jamaa, marafiki na majirani kwenye futari ya pamoja. Baadhi ya nyakati wageni waalikwa hufikia zaidi ya 100 . Waalikwa hao huanza kuwasili kwenye nyumba waliyoalikwa jua linapokaribia kutua na kukuta familia hiyo tayari imefanya maandalizi ya kutosha ya vyakula na mambo yote ya lazima.

Wanafamilia huwa hawaketi jamvi au meza moja na wageni, bali husimama pembeni wakiwa kama wahudumu tu huku wakiwa na sahani zao. Vyakula haviwekwi vyote kwa mpigo, bali huanza hatua kwa hatua. Kwanza huanza kwa kachumbari, ikimalizika, wahudumu huondoa sahani na kuweka vyombo safi kwa ajili ya aina nyengine ya chakula inayofuatia.

Baada ya kachumbari hufuatia supu, mikate na mafuta kidogo, kisha chakula cha kienyeji kiiitwacho sumsa na vyenginevyo. Baada ya hapo watu huchukua mapumziko kwa ajili ya Swala ya Magharib na kujiandaa kwa awamu ya pili.

Hiyo mpenzi msikilizaji inakuwa ni "shitua mbavu" tu, mlo wenyewe khaswa huanza baada ya Swala ya Maghrib. Mlo huu hujumuisha wali na vitoweo vyake, matunda, mbogamboga na vitu vyengine vitamu vya Futari. Yote haya yakiendelea wenyeji huwa wamesimama tayari tayari kuwahudumia wageni wakiwa wameshika mabuli ya chai ya kijani au ya kwaida, kwani kila mlo huambatana na chai. Baadhi ya wenyeji hao kazi yao huwa ni kusafisha meza tu, kwa vile kila mlo unapomalizika meza husafishwa upya na kuwekwa sahani nyengine swafi kwa ajili ya chakula au kinywaji kinachofuatia.

Baada ya futari kumalizika, wageni waalikwa hunyanyua mikono kuwaombea dua wenyeji wao ili Mola mtukufu awape maghfira na baraka.

Baada ya karamu hiyo kumalizika, inakuja zamu ya watoto. Wao huvalia vizuri, kutembea kwa makundi wakipita nyumba hadi nyumba na kugonga milango wakiomba zawadi huku wakiimba. Hiyo si kwa watoto wa kimaskini tu, bali hata wa kitajiri, kwani ni kama sehemu tu ya utamaduni wa Ramdhanai nchini humo.

Swala ya Tareaweh:

Waislamu nchini Uzbekistan huipa umuhimu mkubwa Swala ya Taraweh. Mara baada ya kumalizika kwa karamu ya Futari watu hukimbilia Misikitini kuiwahi Ibada haiyo maalum katika mwezi huu mtukufu, Kwa kawaida Wauzbeki huswali Taraweh kwa Rakaa 20. Wanawake nao huswali Taraweh, wachache hujumuika katika Misikiti ya kawaida, badhi yao katika maeneo maalum kwa ajili yao, na wachache huswali majumbani mwao.

Baada ya Swala ya Taraweh, watu huendelea na vikao vya visomo vya Qur'an, mawaidha au hata mazungumzo yenye faida ikiwemo kujikumbusha historia ya mababu zao na namna ya kurejesha haiba ya nchi yao ili kuweza kuzalisha kizazi kama cha enzi za Imam al-Bukhari

No comments:

Post a Comment

Maoni yako