If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, June 18, 2017

RUTO ACHAMBUA MATAMSHI YA RAILA ALIPOZURU KAJIADO

Na SAMMY WAWERU

NAIBU wa Rais William Ruto amemtaka kinara wa upinzani National Super Alliance (NASA) Raila Odinga kuepuka kutumia maswala ya shamba kama sera ya kujipigia debe achaguliwe wakati wa uchaguzi mkuu Agosti 8, 2017.

William Ruto
Naibu wa Rais William Ruto akihutubu awali. Picha/DPPS

Ruto aidha ameonya matamshi kama hayo ndiyo yataeneza uchochozi na kuwepo kwa ghasia baada ya uchaguzi mkuu ujao.

"Wale ndugu zetu juzi walienda Maasaini, nataka kueleza viongozi wa ODM hiyo lugha ya kusema watu warudi makwao ni siasa za ufukara. Mwananchi yeyote anafaa kuishi sehemu yoyote katika nchi hii bila kuulizwa swali na yeyote," akasema Naibu Rais Ruto akihutubu Jumamosi katika uwanja wa Bukhungu Kakamega wakati Jubilee ikiendesha kampeni zake maeneo ya Magharibi mwa Kenya kusaka kura ya kuchaguliwa Agosti 8.

Mwanzoni mwa wiki hii kinara wa NASA Raila Odinga akinadi sera zake Kitengela Kaunti ya Kajiado alieleza wapiga kura kaunti hii wasikubali kuuza mashamba yao.

Utengano

Hata hivyo Naibu wa Rais William Ruto amekashifu matamshi hayo akisema ni ya kutenganisha Wakenya kwa msingi wa ukabila.
"Kilichoturejesha nyuma mwaka wa 2007 ni siasa kama hizi za ukabila," akasema Ruto.

Naibu huyu wa Rais amesema Raila awache kuendesha siasa za 'ufukara' na badala yake auze sera za kuunganisha wananchi.


"Tunataka yule jamaa wetu wa kitendawili awache siasa za ufukara za kusema watu wahame," akaeleza Bw Ruto akimlenga kiongozi wa ODM Raila Odinga ambaye anapeperusha bendera ya kuwania urais Agosti 8 katika mrengo tanzu wa NASA
.
Ruto amemsuta Raila kuwa aliongea na Rais Uhuru Kenyatta baada ya Agosti 8 ampe pesa za kustaafu akieleza imani yake Jubilee itabwaga NASA.

"Mimi nimeongea na Rais amtafutie (Raila) donge nono atakapostaafu baada ya Agosti 8 kwa sababu nina uhakika tutamshinda," akasema Ruto akihutubu katika uwanja wa Bukhungu, kaunti ya Kakamega.

"Nimesikia kule wanaenda wamehangaika sana na mimi. Wanasema Rais ni mtu mzuri, sasa kama wamekubali Rais ni mzuri si tumpitishe kisha wapatane na mimi mwaka wa 2022," amesema Ruto.

Kinara wa NASA Raila Odinga hii leo akihutubu Mikinduri, Meru wakati akiendesha kampeni za kuvutia ngoma upande wa mrengo wake, amekanusha madai hayo akisema yeye ni kiongozi atakayeleta na kuunganisha makabila yote pamoja wala si kuyatenganisha.

"Sisi tutahakikisha kuna usalama na upendo kwa makabila yote. Walisema ati nilisema nikichukua serikali watu watarudi makwao, warudi kwao waende wapi ilhali hii nchi ni yao?" akataka kujua Raila.

"Wanasema Raila akiwa pale (uongozini) Wameru mtataabika, kwani mimi ndiye adui ya Wameru?" akauliza akauliza umati wa watu uliofika kumsikiliza akiandamana na vinara wenza NASA, akiongeza kuwa yeye (Raila) ndiye alitengeneza barabara nyingi za Meru alipokuwa Waziri wa Barabara na Ujenzi.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako