If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, June 30, 2017

SONKO NA KENNETH WAKWEPA MDAHALO, IGATHE ASEMA NI MTEGO WA KIDERO

Na LEONARD ONYANGO

SENETA wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko na aliyekuwa mbunge wa Gatanga Peter Kennneth Jumatano walikwepa mdahalo uliolenga kuwapa nafasi wawaniaji wa ugavana wa Kaunti ya Nairobi kuelezea sera zao.

Mike Sonko
Seneta Mike Sonko akihutubua wanahabari katika Shule ya Msingi ya Bidii, Buruburu Aprili 26, 2017. Picha/ CHARLES WASONGA

Bw Sonko anayewania ugavana kupitia tiketi ya chama cha Jubilee, badala yake, alituma mwaniaji mwenzake Polycarp Igathe, ambaye alitimuliwa na waandalizi kutokana na kigezo kuwa mdahalo huo ulilenga wagombeaji wa ugavana pekee.

Baada ya kutimuliwa, Bw Igathe, aliambia Taifa Leo kuwa mdahalo huo uliofadhiliwa na Chama cha Wakaaji (KARA) na Chama cha Watengenezaji Bidhaa (KAM), ulikuwa mtego wa Gavana Evans Kidero wa kutaka kumnasa na kumdhalilisha Bw Sonko.


“Mdahalo huo ulilenga kutoa sera zinazowaathiri wakazi wa Nairobi. Hivyo, waandaaji wa mdahalo huo kusisitiza kwamba ni sharti mwaniaji ajitokeze yeye binafsi ni hujuma na ubaguzi,” akasema Bw Igathe.

Bw Igathe alidai kuwa Bw Sonko hakushiriki kwa sababu mdahalo huo wa jana ulikuwa 'duni’. Naye Bw Kenneth ambaye ni mwaniaji huru, hakufika na wala hakutuma udhuru.

Hata hivyo, mdahalo huo ulihudhuriwa na wawaniaji wengine Gavana Kidero (ODM), Miguna Miguna (Mwaniaji Huru), Michael Mutinda (Agano ); Godfrey Wanyoike (Mwaniaji Huru ) na Macharia Kamau (PDU).


Gavana Kidero alikuwa na kibarua kigumu kujitetea baada ya wapinzani wake kumshambulia vikali huku wakisema kuwa ameshindwa kukabiliana na ufisadi, kusafisha jiji na hata msongamano wa magari jijini.

Dkt Kidero alijitetea kwa kusema kuwa ameanzisha mchakato wa kukabiliana na msongamano wa magari jijini kwa kujenga maeneo ya kuegesha matatu katika maeneo ya Muthurwa, Ngara na sehemu nyinginezo.

“Serikali yangu imechukua mikakati mbalimbali ya kukabiliana na maafisa wafisadi. Kwa mfano, nilitimua maafisa 300 waliopatikana wakijihusisha na ufisadi,” akasema Dkt Kidero.

“Tumeanzisha mfumo wa 'ejijipay’ ambapo kodi inaliopwa kupitia simu kwa lengo la kumaliza ufisadi,” akaongezea.
Naye, Bw Macharia aliahidi kuwapa makazi watu wanaoishi katika vitongoji duni.

“Inasikitisha kuwa watu wanaishi katika mazingira duni ilhali simba wachache wanaishi katika Hifadhi ya Nairobi ilhali maelfu ya watu wanaishi katika mitaa ya mabanda. Nikichaguliwa kuwa gavana wa Nairobi nitabadili hifadhi ya Nairobi kuwa makazi ya watu kutoka Kibera na mitaa mingineyo ya mabanda,” akasema Bw Macharia.

Bw Miguna aliahidi kujenga barabara za kisasa jijini Nairobi kwa lengo la kumaliza tatizo la msongamano wa magari.

Bw Mutinda aliahidi kuondoa mizunguko ya magari katika maeneo yote katikati mwa jiji. Bw Wanyoike aliahidi kutoa kitita cha Sh2 billioni kwa wafanyabiashara wadogo jijini Nairobi kila mwaka iwapo atachaguliwa kuwa gavana.

Mdahalo huo, pia ulisheheni sarakasi tele ambapo Bw Miguna alidai kuwa Gavana Kidero ni kibaraka cha Jubilee ndani ya muungano wa NASA.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako