If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, June 6, 2017

THERESA MAY ATANGAZA VITA VIKALI KUTOKOMEZA MAGAIDI UINGEREZA

Na MWANGI MUIRURI na MASHIRIKA

WAZIRI Mkuu wa Uingereza Bi Theresa May amesema kuwa liwe liwalo, kero la ugaidi katika ardhi yake lazima limalizwe.

Theresa May
Waziri Mkuu wa Theresa May ahutubu Juni 5, 2017 katika uwanja wa Odsal, Bradford, West Yorkshire. Uchaguzi ni Juni 8, 2017. Picha/AFP

Ametangaza hayo katika kipindi cha saa 72 baada ya taifa hilo kugongwa na shambulio la kigaidi ambapo wavamizi walipenya hadi kwa raia wakitumia lori lililokuwa na vilipuzi na kuwaua watu saba na kuwajeruhi wengine 48.


Hatimaye, wavamizi hao waliokisiwa kuwa watatu walishuka kutoka kwa lori hilo na kuanza kushambulia raia kwa visu.

Shambulio hilo lilitekelezwa katika eneo la London Bridge na kisha katika baa moja iliyo karibu.

Hili lilikuwa shambulio la tatu katika kipindi cha miezi mitatu.

Hata hivyo, May alitangaza kuwa uchguzi mkuu wa taifa hilo wa Alhamisi utaendelea kama ulivyoratibiwa lakini katika mazingara ya onyo kuwa “tumekuwa walegevu sana kuhusu kero hili na sasa ni wakati wa kutoa makali yetu yote kama taifa dhidi ya dhana potovu kuwa hasira ya hasara ya magaidi ni sharti iangamizwe hapa Uingereza.”

Amesema May: “Ni wakati wa kutangaza kwa kauli moja iliyo wazi na ikilenga mitandao yote ya ugaidi kuwa Uingereza imeamua hayo tosha kwa sasa.”


Huku bendera za taifa hilo zikipeperushwa nusu mlingoti, alisema “ni wakati wa kusema hatutakaa kwa unafiki wa kufikiria hali itajipa suluhisho yenyewe. Tuko katika vita sasa na ugaidi na pia dhidi ya waigizaji wa ugaidi ambao wakihisi kumwaga damu wanatumia mbinu za kigaidi katika ardhi yetu.”

Ngome za IS

Mtandao wa Islamic State, ambao kwa sasa unafurushwa kutoka ngome zake katika mataifa ya Syria na Iraq chini ya makali ya kijeshi ya Marekani tayari umekiri kuhusika katika shambulizi hilo Uingereza.

Tayari, idara ya polisi Uingereza imetangaza kuwatia mbaroni washukiwa 12 kuhusiana na shambulizi hilo.

Ni wiki mbili sasa zimepita tangu shambulio lingine la kigaidi katika taifa hilo liliwaua watoto 22 katika hafla ya utumbuizaji ya msanii wa Marekani Ariana Grande katika eneo la Manchester Kaskazini mwa taifa hilo.

May ametangaza kuwa “mitandao hii inayotumia uongo wa kudhalalisha dini ya Kiislamu itakabiliwa mchana na usiku, mitaani na nyumbani na katika mitandao ya Intaneti.”

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako