If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, June 24, 2017

Umoja wa Mataifa kutuma wataalamu wa Kimataifa, Kasai, DRC

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kutuma wataalamu wa kimataifa katika eneo la Kasai la katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa lilitoa azimio mjini Geneva Uswisi na kusema kuwa, umoja huo umeamua kutuma wataalamu wa kimataifa nchini Kongo kwa ajili ya kuchunguza mapigano na machafuko yaliyotokea katika eneo la Kasai.

Aidha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limemtaka Zeid Ra’ad Al Hussein, kamishna mkuu wa haki za binadamu wa umoja huo atoe ripoti ya uchunguzi huo katika kikao cha kawaida cha 37 cha baraza hilo.

Makaburi ya umati katika eneo la Kasai, DRC

Makanisha ya Kikatoliki yamesema kuwa, zaidi ya watu elfu tatu wameshauawa hadi hivi sasa tangu yalipozuka mapigano katika eneo la Kasai mwaka jana.

Umoja wa Mataifa aidha umesema kuwa, watu milioni 1.3 wameyakimbia makazi yao katika eneo hilo la katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na machafuko hayo. Watu 30 elfu wamekimbilia katika nchi jirani ya Angola.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako