If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, June 8, 2017

Waingereza washiriki uchaguzi mkuu, Wabunge 650 kuchaguliwa

Mamilioni ya wananchi wa Uingereza hii leo wanaelekea kwenye masanduku ya kupiga kura kushiriki uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, ambapo chama tawala cha Kihafidhina kinatazamiwa kuchuana vikali na chama cha upinzani cha Leba.

Wabunge 650 wanatazamiwa kuchaguliwa katika zoezi hilo, ambapo takriban watu milioni 46.9 wametimiza masharti ya kupiga kura. Chama kitakachozoa kura nyingi kitajipatia fursa ya kuunda serikali ijayo ya Uingereza.

Ushindani mkali uko kati ya chama tawala cha Kihafidhina kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa sasa Theresa May na kile cha upinzani cha Leba kinachoongozwa na Jeremy Corbyn.

Corbyn amekuwa akisisitiza kuwa, ni katika manifesto ya chama chake kulitambua mara moja taifa la Palestina iwapo wataibuka na ushindi katika uchaguzi huu wa mapema, sambamba na kushinikiza kusitishwa mara moja mzingiro wa kibaguzi, ukaliaji wa mabavu wa ardhi za Wapalestina na kuendelezwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina.

Thereza May (kulia) na Jeremy Corbyn

Uchaguzi huu unafanyika chini ya anga ya mashambulizi ya kigaidi yaliyoshuhudiwa hivi karibuni katika baadhi ya miji ya nchi hiyo. Shambulizi la hivi karibuni ni lile la Jumamosi iliyopita, ambapo magaidi watatu waliua watu saba katika tukio lililohusisha watu kugongwa na gari na wengine kuchomwa visu jijini London. 


Tukio hilo lilitokea majuma kadhaa tu baada ya watu 22 kuuliwa baada ya gaidi kujiripua ndani ya uwanja mmoja wa burudani mjini Manchester.

Ni vyema kuashiria hapa kuwa, uchaguzi huu ulipasa kufanyika mwezi Mei mwaka 2020, lakini mwezi jana Theresa May aliitisha uchaguzi wa kabla ya wakati.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako