If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, June 18, 2017

Waislamu wazidi kunyanyaswa nchini Uingereza

Vitendo vya unyanyasaji dhidi ya Waislamu vimeongezeka nchini Uingereza hasa baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi katika miji ya Manchester na London.

Gazeti la al Quds al Arabi linalochapishwa mjini London limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, licha ya Waislamu wa Uingereza kulaani vikali mashambulizi hayo ya kigaidi na kusisitiza kwamba vitendo hivyo ni kwa madhara ya jamii ya Uingereza wakiwemo Waislamu, lakini pamoja na hayo, unyanyasaji dhidi ya Waislamu umeongezeka.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Manispaa ya London, vitendo vya unyanyasaji dhidi ya Waislamu vimenogezeka mara tano tangu yalipotokea mashambulio ya kigaidi mjini humo.

Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza, Mohammad Kozbar

Naye Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Uingereza Mohammad Kozbar, ameliambia gazeti la al Quds al Arabi kwamba, inasikitisha kuona kuwa Waislamu ndio wanaolipiziwa kisasi cha mashambulio ya kigaidi licha ya kwamba wanapinga vikali mashambulizi hayo.

Amesema, kuvunjiwa heshima misikiti, kutumiwa Waislamu ujumbe wa vitisho na wa kulipiza kisasa kwenye mitandao ya kijamii n.k, ni miongoni mwa unyanyasaji wanaofanyiwa waziwazi Waislamu.

Amesema, hayo yote yanatokana na ujinga uliotanda katika jamii ya Uingereza kuhusiana na dini tukufu ya Kiislamu, hivyo kuna wajibu wa kufanyika jitihada kubwa zaidi za kuonyesha sura halisi ya Uislamu na kupinga kikamilifu vitendo vyote vya kigaidi vinavyohusishwa na dini hiyo ya Mwenyezi Mungu.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako