If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, June 7, 2017

WAKENYA WAMESAHAU UFISADI KUTOKANA NA NJAA - RIPOTI

Na VALENTINE OBARA

NJAA na gharama ya juu ya maisha zimefanya wananchi kusahau janga la ufisadi linalokumba taifa, utafiti umeonyesha.

Hongo
Mkenya akimpokeza mwenzake pesa. Picha/ HISANI

Matokeo ya utafiti uliofanywa na shirika la Ipsos yamebainisha idadi kubwa ya Wakenya wanaamini njaa na bei ghali ya bidhaa muhimu ndiyo matatizo makuu zaidi yanayokumba nchi, ikilinganishwa na ufisadi.

Utafiti huo uliofanywa kati ya Mei 11 hadi Mei 23, unaonyesha asilimia 36 ya wananchi walitaja gharama kubwa ya maisha kuwa tatizo linalokumba nchi, huku kukiwa na asilimia 21 wanaoamini njaa ndiyo tatizo kuu.

Kwa upande mwingine, ufisadi ulitajwa na asilimia 15 pekee ya Wakenya, ikifuatwa na asilimia 13 waliosema tatizo kuu ni ukosefu wa ajira.

Hali hiyo ni tofauti na ilivyokuwa Januari ambapo asilimia 21 walikuwa wanaamini ufisadi ndio tatizo kuu, na asilimia 14 pekee wakati huo walisema njaa inatatiza zaidi.

Hata hivyo, mchanganuzi wa utafiti katika shirika la Ipsos, Dkt Tom Wolf, alisema matokeo hayo hayamaanishi Wakenya wamesahau changamoto ya ufisadi unaokumba nchi.


“Ni vile tu suala hilo halijapewa uzito ikilinganishwa na masuala mengine kama vile ukame na ukosefu wa chakula cha kutosha. Fauka ya hayo, huenda ni kutokana na jinsi vyombo vya habari haviangazii ufisadi zaidi wakati huu,” akasema, kwenye taarifa kwa vyumba vya habari.

Wengi waliohojiwa (asilimia 48) walisema hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kukabiliana na njaa.
Asilimia 23 walisema kumekuwa na juhudi za kusambaza vyakula vya misaada, na asilimia 16 wakasema maji yamesambazwa kupunguza athari za hali hiyo.

Hata hivyo itakumbukwa utafiti ulifanywa kabla serikali itekeleze kikamilifu juhudi kadhaa kama vile kupunguza bei ya unga wa mahindi.

Utafiti pia ulionyesha Nairobi inaongoza kwa idadi ya wanaokabiliwa na umasikini (asilimia 52), ikifuatwa na Pwani, Nyanza na Rift Valley kwa asilimia 46 kila eneo.

Asilimia 45 ya waliohojiwa walisema hali hii inaweza kutatuliwa kwa kuongeza nafasi za ajira.
Dkt Wolf alisema ajenda zinazolenga kutatua changamoto hizo huenda zikategemewa na wapigakura kufanya maamuzi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako