If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, July 5, 2017

Algeria: Waafrika elfu tano wamejiunga na makundi ya kigaidi

Rais wa Algeria ametahadharisha kuhusu hatari ya vijana elfu tano wa Afrika waliojiunga na mkundi ya kigaidi.

Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ameyasema hayo katika ujumbe wake uliosomwa kwenye mkutano wa viongozi wa Afrika unaofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia na kuongeza kuwa: Vijana wengi wa nchi za Afrika wamejiunga na makundi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali duniani hususan Iraq, Syria na eneo la Sahel kaskazini mwa Afrika.

Amesema kuwa, nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na uwezekano wa magaidi wa Kiafrika kurejea katika nchi zao na ametoa wito wa kuwepo ushirikiano katika masuala ya kiusalama na upelelezi kwa ajili ya kudhibiti vyema mipaka na kuzuia harakati za magaidi.

Mkutano wa AU, Addis Ababa

Kwa miaka kadhaa sasa makundi ya kigaidi kama Daesh yaliyoanzishwa kwa ufadhili na misaada ya hali na mali ya Marekani, Saudi Arabia, Israel na washirika wao yamekuwa yakifanya mashambulizi katika nchi mbalimbali duniani hususan katika nchi za Syria na Iraq. Makundi hayo yamesajili wapiganaji kutoka nchi nyingi zikiwemo za Afrika.

Mkutano wa 29 wa viongozi wa nchi za Afrika ulianza jana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Zaidi ya viongozi 25 wa nchi za Afrika wanahudhuria mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako