If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, July 23, 2017

Chama cha Merkel chapinga sheria ya ndoa baina ya watu wenye jinsia moja

Wawakilishi wa chama cha Christian Democratic Union (CDU) kinachoongozwa na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel wamepinga vikali hatua ya kupasishwa sheria inayoruhusu ndoa baina ya watu wenye jinsia moja nchini humo na kutangaza kuwa, watawasilisha mashtaka katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo.

Chama cha CDU kimekuwa kikipinga ndoa za aina hiyo na kiongozi wake, Angela Merkel alitangaza waziwazi kuwa anapinga suala hilo ingawa aliwaruhusu wabunge wa chama hicho kupiga kura bungeni kwa mujibu wa mitazamo yao binafsi.

Wabunge 225 kati ya 309 wa chama cha Christian Democratic Union walipiga kura ya hapana dhidi ya muswada wa sheria hiyo.

Sheria inayoruhusu ndoa baina ya watu wenye jinsia moja nchini Ujerumani ilitiwa saini juzi na Rais Frank-Walter Steinmeier wa nchi hiyo na itaanza kutekelezwa rasmi Oktoba Mosi mwaka huu.

Wajerimani wakiandamana kupinga ndoa baina ya watu wenye jinsia moja

Ikumbukwe kuwa, mwezi uliopita wa Juni, Bunge la Ujerumani, Bundestag liliipasisha sheria inayoruhusu ndoa za watu wa jinsia moja na kutambua rasmi eti haki ya watu wanaojihusisha na ngono ya jinsia moja kulea watoto nchini humo.

Kwa utaratibu huo, sasa Ujerumani inakuwa nchi ya 21 ya bara Ulaya kupasisha sheria ya ndoa baina ya watu wenye jinsia moja. Denmark ndiyo iliyokuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kupasisha sheria kama hiyo mwaka 1992

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako