If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, July 21, 2017

IEBC IMEKODI WATAALAMU WA KUZUIA MITAMBO YAKE KUDUKULIWA

Na CHARLES WASONGA

TUME huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Ijumaa, Julai 21, 2017, iliondoa hofu ya uwezekano wa mitambo yake ya kielekroniki kudukuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 8.

Roselyne Akombe
Roselyne Akombe ni kamishna wa IEBC. Picha/MAKTABA

Kamishna wa tume hiyo Roselyn Akombe alisema wamekodi huduma za kampuni kubwa za kiteknojia ambazo zitaisaidia kuzuia uhalifu huo.

“Tumewaaleta wataalamu waliobobea katika vita dhidi ya uhalifu wa kimtandao. Wanatoka kampuni maarufu kama vile, Oracle, Dell na IBM na watatusaidia kukabiliana na hatari hii endapo itapenyeza katika mitambo yetu siku ya uchaguzi,” akasema.

Dkt Akombe alisema hayo wakati wa kongamano kuhusu usimamizi wa uchaguzi mkuu ulioandaliwa na mashirika ya kijamii, katika mkaha wa Intercontinentali, Nairobi.

Mkutano huo pia ulihudhuria na waangalizi wa uchaguzi na wanahabari miongoni mwa dau wengine katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Kamishna huyo alisema mitambo ya kutambua wapigakura kieletroniki na ile ya kutuma matokea ya uchaguzi itafanyiwa majaribio kuanzia Julai 31 “ili kuhakikisha kuwa inafanyakazi vizuri wakati wa uchaguzi mkuu Agosti 8”.

“Shughuli hiyo itaendeshwa katika vituo mbalimbali vya kupigia kura kote nchini. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila kitu ki sawa Agosti 8,” Dkt Akombe akawaambia washiriki katika kongamano hilo.


Hakikisho hilo linajiri siku moja baada ya wabunge watatu wa Jubilee kudai kuwa Muungano wa Upinzani, NASA, unapanga kudukua mitambo ya kieletroniki ya IEBC kwa lengo la kuiba kura.

Wabunge hao Kimani Ichung’wa (Kikuyu), Moses Kuria (Gatundu Kusini) na Seneta Mteule Bi Beatrice Elachi walikuwa wakiongea na wanahabari katika makao makuu ya chama cha Jubilee mtaa wa Pangani, Nairobi.

“Tunafahamu kuwa NASA imepata usaidizi kutoka Tanzania kwa nia ya kudukua mitambo ya IEBC. Hii ndio maana wameanzia kituo cha kujumuisha kura katika taifa hilo jirani, “ akasema Bw Ichung’wa.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako