If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, July 4, 2017

ISIS yawafanya wakimbizi wakazi laki tisa wa Mosul, Iraq

Waziri wa Uhamiaji wa Iraq amesema kuwa, uvamizi na uharibifu mkubwa uliofanywa na genge la kigaidi la Daesh ambao umelilazimisha taifa zima la Iraq kusimama na kuendesha mapambano ya kuukomboa mji wa Mosul wa kaskazini mwa nchi hiyo, umesababisha zaidi ya wakazi laki tisa wa mji huo kuwa wakimbizi.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Dk Jassim Mohammed al Jaaf, waziri wa whamiaji na masuala ya mananchi maliopoteza makazi yao nchini Iraq akisema hayo leo na kuongeza kuwa, watu laki tisa na 857 wamekimbia makazi yao huko Mosul tangu ilipoanzia opereseheni ya kuukomboa mji huo tarehe 17 Oktoba 2016 hadi hivi sasa na kwamba laki moja na 76,455 ni wakazi wa mashariki mwa mji huo na laki saba na 24,402 ni wakazi wa magharibi mwa Mosul.

Raia wa kawaida hasa watoto wadogo ni wahanga wakuu wa jinai za magaidi wa Daesh nchini Iraq

Amesema, wakimbizi laki tano ambao ni sawa na asilimia 64 ya wakimbizi hao wamepewa makazi katika kambi maalumu zilizoandaliwa na wizara yake na hadi hivi sasa watu laki mbili na 17,854 wamesharejea kwenye maeneo yao huko Mosul baada ya kufurushwa magaidi wa Daesh.

Ikumbukwe kuwa, Alkhamisi iliyopita, wizara ya ulinzi ya Iraq ilitoa tamko na kutangaza kukombolewa mji wa Mosul kutoka kwenye makucha ya magaidi wakufurishaji wa Daesh (ISIS).

Baada ya vikosi vya ulinzi vya Iraq kwa kushirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi maarufu kwa jina la Hashdu Shaabi kukombowa upande wa mashariki mwa mji wa Mosul mwezi Februari 2017, vikosi hivyo vilianzisha operesheni ya kukomboa upande wa magharibi mwa mji huo ambapo siku ya Alkhamisi iliyopita, operesheni ya kuukomboa mji huo ilimalizika.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako