If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, July 24, 2017

Jamhuri ya Kongo na uchaguzi wa Bunge

Katika hali ambayo duru ya kwanza ya uchaguzi wa Bunge nchini Congo Brazaville ilifanyika tarehe 16 mwezi huu wa Julai; raia wa nchi hiyo hivi sasa wanajiandaa kuelekea katika masandukuru ya kupigia kura kwa ajili ya duru ya pili ya uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 30 mwezi huu.

Chama cha Labour cha nchini Kongo anachotoka Rais Dennis Sassou Nguesso wa nchi hiyo kilipata ushindi mkubwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa uliofanyika tarehe 16 mwezi huu kwa kupata viti 70 vya uwakilishi kati ya jumla ya viti 151 vya bunge la nchi hiyo. 

Hii ni katika hali ambayo karibu asilimia 30 ya wagombea wa chama hicho pia wameingia katika duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa bunge.

Matokeo ya duru hiyo ya awali ya uchaguzi wa bunge yanaonyesha kuwa wagombea binafsi saba ambao walitangaza utiifu wao kwa chama cha Union of Humanist Democrats (UDH-Yuki) wanashika nafasi ya pili baada ya wagombea wa chama tawala cha Labour. 

 Chama cha UDH-Yuki kinaoongozwa na Guy- Brice Parfait Kolelas shakhsia wa upinzani wa huko Kongo Brazaville ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi wa rais wa mwaka jana. Duru ya pili ya uchaguzi wa bunge nchini humo imepangwa kufanyika tarehe 30 mwezi huu wa Julai.

Guy-Brice Parfait Kolelas, Mkuu wa chama cha upinzani cha UDH-Yuki akizungumza na vyombo vya habari

Chama cha Labour kimekuwa madarakani tangu mwaka 1997. Hilo ndilo lililompelekea Rais Sassou Nguesso aweze kusogeza mbele malengo na mipango yake katika kalibu ya bunge na kwa njia za kisheria. 


Moja ya mipango hiyo ni pale mwaka uliopita ambapo Rais huyo wa Jamhuri ya Kongo aliweza kuidhinisha kufanyiwa marekebisho katiba ya nchi hiyo baada ya kuungwa mkono na kura nyingi za wabunge kutoka chama tawala cha Labour; na kwa mara nyingine tena kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka uliopita baada ya kuondoa vizuizi na masharti kuhusu umri na muda kwa watu wanaostahiki kugombea kiti cha urais. 

Denis Sassou Nguesso alitangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais mwaka jana baada ya kupata karibu asilimia 60 ya kura zote huku vyama vinavyoipinga serikali vikitilia shaka uwazi wa uchaguzi huo vikisema kuwa kulifanyika udanganyifu mkubwa.

Rais Denis Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Kongo Brazaville

Hali ya mgogoro na ghasia za kisiasa imeendelea kutawala huko Congo Brazaville licha ya kupita miezi kadhaa sasa tangu kufanyike uchaguzi wa rais mwaka uliopita. Wakati huo huo Huu ni uchaguzi wa kwanza wa bunge kufanyika huko Congo Brazaville baada ya kufanyiwa marekebisho katiba ya nchi hiyo. 

Hata kama kwa mara nyingine tena chama tawala cha Labour ndicho chenye viti vingi vya uwakilishi bungeni, lakini vyama vya upinzani vinataraji kwamba vyama na taasisi za kiraia zitaweza kufuatilia matakwa yao kwa mujibu wa sheria katika anga ya kisiasa iliyopo kufuatia marekebisho yaliyotekelezwa. Kukomeshwa machafuko na kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa ni moja ya matakwa muhimu ya wapinzani katika Jamhuri ya Kongo. 

Miezi kadhaa iliyopita makumi ya wapinzani walitiwa mbaroni kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na hivi sasa wamefungwa jela. Vyama vya upinzani aidha vinataka raia wawe huru na vile vile kuwepo na uhuru wa kujieleza nchini humo.

Kuboreshwa hali ya uchumi ni moja ya matakwa mengine makuu yanayotiliwa mkazo na vyama na raia wa Jamhuri ya Kongo. Congo Brazaville miaka kadhaa iliyopita ilikabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi, uhaba wa chakula, umaskini, ufisadi na kupanda kwa gharama ya maisha kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta duniani kwa upande mmoja; na kwa kwa upande wa pili nch hiyo kukabiliwa na harakati za makundi ya wanamgambo na wimbi la wakimbizi katika mipaka ya pamoja na nchi zilizoathiriwa na migogoro na vita kama vile Jamhuri ya Afrika ya Kati. Hii ni katika hali ambayo Congo Brazaville ni nchi yenye utajiri mkubwa wa maliasili na madini mbalimbali huku ikidhamini asilimia 30 ya dhahabu na almasi duniani.

Wananchi wa Jamhuri ya Kongo wanataraji kuwa hali ya mambo nchini kwao itaboreka na mijadala ya kisiasa kupungua baada ya kumalizika uchaguzi huo wa bunge na kuanza kazi bunge jipya nchini.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako