If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, July 20, 2017

KAMA NASA HAIKO TAYARI KWA UCHAGUZI, ISUBIRI 2022 NIPAMBANE NAO - RUTO

Na DANIEL NYASSY

Bw Ruto alimtetea Dkt Matiang’i akisema ana haki ya kukutana na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kupanga usalama wa wapiga kura.

Naibu Rais William Ruto
Naibu Rais William Ruto akihutubu awali. Picha/MAKTABA

Akiongea Changamwe, Mombasa, Bw Ruto aliwataka viongozi wa NASA kutangaza iwapo wako tayari kwa uchaguzi wa Agosti 8 ama la.

“Watangaze msimamo wao; wako tayari kwa uchaguzi huu ama hawako tayari? Kama hawako tayari wangojee uchaguzi wa 2022 nipambane nao,” alisema.

Aliwapatia changamoto endapo wanataka kuwa maafisa wa Tume huru ya Uchaguzi IEBC ama wagombea kwenye uchaguzi huo wa mwezi ujao.

“Hawa wangwana waachane kabisa na Matiang’i na wapambane na Rais Kenyatta na mimi. Wanadai Matiang’i anafanya siasa lakini hafanyi siasa, sisi tuna watu wa kutosha kutufanyia siasa,” alisema.

Alisema Dkt Matiang’i hana haja ya kufanya uamuzi wowote kuhusu uchaguzi huo bali ni wao wanahitaji kuamua kama wako tayari kwa uchaguzi au la.

Alisema upinzani unatumia muda mwingi kudai kwamba wanalinda kura zao lakini akapuuzilia mbali usemi huo akisema, kura za upinzani ni finyu.


“Hawa jamaa wanapoteza muda mwingi kusema eti wanalinda kura zao. Lakini huwezi kulinda usichokuwa nacho. Hata ukilinda kura hizo ambazo ni kidogo kwa masaa 24 kila siku, haziwezi kuongezeka,” akasema Bw Ruto.

Aliwaambia viongozi hao kujishughulisha zaidi na kusaka kura miongoni mwa wananchi badala ya kusema wanalinda kura.

Aliutaka upinzani kuondoa kesi zilizo mahakamani kuhusiana na uchaguzi akisema viongozi wake wanatumia mahakama uchaguzi uahirishwe.

“Waondoe kesi chungu mzima zilizoko mahakamani ambako walikwenda kujaribu kusimamisha uchaguzi,” alisema.

Bw Ruto aliandamana na Rais Uhuru Kenyatta.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako