If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, July 13, 2017

KIPINDI CHA BARIDI KUENDELEA JULAI

Na CAROLYNE AGOSA

BARIDI kali inatarajiwa kuendelea kukumba maeneo mengi nchini huku Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ikisema kuwa sehemu kadha zitashuhudia nyuzi chini ya 10°C.

Mvua ya ghafla
Wakazi wa Eldoret wahangaishwa na mvua ya ghafla Septemba 1, 2015. Picha/JARED NYATAYA

Katika tathmini ya mwezi Julai, idara hiyo imewataka wananchi kuvaa mavazi mazito kwani mwezi huu hushuhudia visa vingi vya maradhi ya kupumua kama vile homa kali na pumu.

Nairobi na miji mingine ya eneo la kati itakumbwa na ukungu mwingi utakaoathiri usafiri wa barabarani na angani.

“Nyanda za juu za bonde la ufa (Nyeri, Muranga, Kiambu, Embu, Meru) na eneo la Nairobi (Dagoretti, Wilson, Eastleigh) zitashuhudia baridi, mawingu na ukungu huku mvua za rasharasha zikinyesha,” alisema mkurugenzi wa idara hiyo Bw Peter G. Ambenje kwenye tathmini ya mwezi Julai.

“Siku kadha kutakuwa na baridi kali huku joto la juu kabisa mchana likiwa chini ya nyuzi 20, na chini zaidi wakati wa usiku likishuka hadi chini ya nyuzi 10.”

Idara hiyo imewaomba madereva kutahadhari kwani kuna uwezekano wakakosa kuona vizuri barabarani.


“Madereva hasa kwenye barabara ya Limuru-Naivasha wanashauriwa kuwa waangalifu zaidi ili kuzuia ajali. Ukungu pia utaathiri safari za ndege katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta,” akasema Bw Ambenje.

Wananchi pia wametahadharishwa dhidi ya kupumua gesi yenye sumu ya jiko la makaa katika harakati za kuota moto.

Alieleza Bw Ambenje: “Watu wanashauriwa wasitumie jiko la makaa ndani ya nyumba zisizo na madirisha ya kutosha kuingiza hewa, wasije wakapumua gesi hatari ya Carbon monoxide.

“Visa vya maradhi ya kupumua kama vile homa, pumu na nimonia vitaongezeka kutokana na baridi kali itakayokuwepo. Watu wanafaa kuvalia mavazi ya kuzuia baridi ili kujiepusha na maradhi hayo.”
Kwa ujumla, maeneo mengi nchini yatakuwa kavu huku mvua ikinyesha eneo la Magharibi na Pwani pekee.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako