If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, July 11, 2017

Mishahara ya wanasiasa nchini Kenya yapunguzwa

Na Victor Melkizedeck Abuso 

Tume ya kusawazisha mishahara nchini Kenya imepunguza mishahara ya wanasiasa nchini humo kulekea Uchaguzi Mkuu tarehe nane mwezi ujao.

media
Jengo la Bunge nchini Kenya
Wikipedia

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Sarah Serem amesema hatua hiyo itasaidia kupambana na ongezeko la bajeti ya kulipa mishahara lakini pia itaisadia serikali kuhifadhi Shilingi za Kenya Bilioni 8 kila mwaka.

Rais Uhuru Kenyatta akiwahotubia Wakenya Jumanne asubuhi, aliunga mkono punguzo hilo na kuwataka raia wa nchi hiyo kuiunga mkono Tume hiyo.

Kenyatta anayewania urais kwa muhula wa pili, ametumia nafasi hiyo kuwaambia wanasiasa kuwa jukumu lao kubwa ni kuwatumia wananchi wala sio kufanya biashara na kupata mishahara mikubwa.

Mshahara wa rais ambao umekuwa ni Shilingi Milioni 1 nukta 6 za Kenya, umepunguzwa hadi Milioni 1 nukta 4.

Magavana wanaoongoza Kaunti mbalimbali watalipwa Shilingi 924,000 kutoka Shilingi 1,056,000.


Wabunge wanaonekana waathirika wakubwa baada ya mshahara wao kuamuliwa kwua sasa utakuwa ni Shilingi 621,250 kutoka Shilingi 710,000.

Kuanzia bunge lijalo, wabunge hawatakuwa na posho wanapokuwa bungeni lakini pia hawatapewa mkopo wa gari.

Kenya inaendelea kufahamika miongoni mwa mataifa ya Jumuiya ya Madola, inayoongoza kwa kuwalipa kiasi kikubwa cha fedha kwa wanasiasa nchini humo hasa wabunge.

Chanzo: sw.rfi.fr

No comments:

Post a Comment

Maoni yako