If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Thursday, July 6, 2017

Mkuu wa Polisi Tanzania kuzungumzia mauaji ya mkoani Pwani

Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania, Simon Sirro amesema hivi karibuni atazungumza kuhusu suala la mauaji yanayotokea mkoani Pwani.

Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, IGP Sirro ameongeza kuwa, Watanzania hawajazoea mambo ya fujo fujo na kwamba wale waliotumwa kwa ubaya watajibiwa vikali.

Watu takribani 37 wamepoteza maisha tangu Mei mwaka jana yalipoibuka mauaji ya kutumia risasi katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani. Kati ya waliouawa katika hujuma hizi ni askari wa polisi na viongozi wa serikali za mitaa.

Maafisa wa Polisi Tanzania

Jeshi la Polisi Tanzania hivi karibuni lilitangaza kuunda Kanda Maalumu ya Rufiji ili kukabiliana na mauaji katika eneo hilo. 

Aidha jeshi hilo limesema limeua watu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wauaji na kutangaza majina yawengine 16 linaowasaka kwa tuhuma za kuendesha vitendo hivyo. 

Aidha IGP Sirro ametoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa kamanda mpya wa Kanda Maalumu ya Rufiji ili kuhakikisha mauaji hayo yanakwisha.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako