If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, July 14, 2017

Mwanadiplomsia Mkongwe Kenya, Bethuel Kiplagat, afariki

Mwanadiplomasia mkongwe nchini Kenya, Bethuel Kiplagat, amefariki dunia ikiwa ni katika msururu wa vifo vya maafisa wa ngazi za juu nchini humo siku za hivi karibuni.

Kiplagat ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Haki na Maridhiano Kenya TJRC amefariki dunia leo katika Hospitali ya Nairobi akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Balozi Kiplagat aliwahi kuhudumu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya kama balozi wa nchi hiyo Uingereza na Ufaransa kabla ya kuteuliwa kuwa katibu wa kudumu katika wizara hiyo.

Alihudumu pia kama mjumbe maalum wa Kenya katika mpango wa amani nchini Somalia kati ya 2003 na 2005 na kuongoza bodi ya hazina ya utafiti wa matibabu barani Afrika kutoka 1991 hadi 2003.

Aliwahi kuhusishwa na mauaji ambapo mamia ya raia wa Wajir waliuawa, huku wengine wakiteswa wakati wa operesheni ya usalama.

Mnamo mwezi Agosti 2016, Kiplagat alimuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka kufanya uchunguzi wa kina baada ya kutajwa katika ripoti ya TJRC.

Kifo cha Kiplagat kinakuja huku Wakenya wakiendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa waziri wa usalama wa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta, Joseph Nkaissery na mawaziri wawili wa zamani Nicholas Biwott na GG Kariuki ambao waliwahi kuhudumu katika serikali ya Rais Daniel arap Moi.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako