If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, July 17, 2017

NIKO TAYARI KUMWAKILISHA NAIBU RAIS KWA MDAHALO - ICHUNG'WA

Na VALENTINE OBARA

NAIBU Rais William Ruto, huenda asihudhurie mjadala wa wagombea wenza wa urais uliopangiwa kufanyika Jumatatu.

Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung'wa
Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung'wa akihutubu awali. Picha/JOSEPH KANYI

Mkurugenzi wa mawasiliano ya dijitali katika afisi ya rais, Bw Dennis Itumbi, pamoja na mbunge wa Kikuyu Bw Kimani Ichung'wa, Jumapili walisema kwamba Bw Ruto ataandamana na Rais Uhuru Kenyatta kwa kampeni maeneo ya Pwani.

“Naibu wa rais atajumuika na bosi wake kwenye kampeni za kisiasa katika Kaunti za Lamu na Tana River Jumatatu,” akasema Bw Itumbi, kwenye taarifa aliyotoa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Bw Ichung'wa alithibitisha hayo, kupitia akaunti yake ya Facebook, akisema kwamba yuko tayari kuukabili muungano wa NASA “na uongo ambao umekuwa ukiwaambia Wakenya.”

“Niko tayari kumkabili Kalonzo Musyoka (ama kinara yeyote wa NASA) kwa niaba ya Naibu Rais, ambaye yuko katika kampeni eneo la Pwani. Ninajihisi mwenye nguvu kutekeleza wajibu huo kwa niaba ya chama changu (Jubilee),” akasema.

Dalili za Bw Ruto kukosa kuhudhuria mjadala huo zilianza kuonekana wiki iliyopita, alipoashiria kwamba hajapokea mwaliko rasmi kutoka kwa waandalizi.

Katika mtandao wake wa Twitter, naibu wa rais alionekana kushangaa kwamba kuna mjadala wa wagombea wenza unaofaa kufanyika.

“Nimeona taarifa za habari zilizochipuka kwamba kutakuwa na mjadala wa wagombea wenza. Ni kweli?” akauliza.


Alitarajiwa kukutana ana kwa ana na mgombea mwenza wa urais kwa muungano wa NASA Bw Kalonzo Musyoka, ambaye kufikia wakati wa kuchapisha gazeti haikuwa imebainika kama atahudhuria.

Mwenyekiti wa kamati simamizi ya mijadala hiyo, Bw Wachira Waruru, Jumapili alinukuliwa kusema wagombea wenza wote walialikwa lakini hakuna aliyethibitisha kama atahudhuria.

Wengine ni wagombea wenza Eliud Kariara wa mgombeaji urais Japheth Kavinga, Emmanuel Nzai (Dkt Ekuru Aukot), Joseph Orina Momanyi (Bw Cyrus Jirongo), Miriam Mutua (Bw Michael Wainaina), Moses Marango (Bw Joseph Naga) na Titus Ng’etuny (Abduba Dida).

Wiki mbili zilizopita, waandalizi wa mijadala ya wagombeaji urais walipata pigo baada ya Rais Kenyatta na mgombeaji urais kwa muungano wa NASA Bw Raila Odinga, kukataa kuhudhuria kwa kulalamikia mfumo uliopangiwa kutumiwa.

Mjadala huo ulikuwa umepangiwa kufanyika Julai 10, katika Chuo Kikuu cha Katoliki (CUEA) na kuhudhuriwa na wagombeaji wote wa urais lakini ukaahirishwa hadi Julai 24.

Mijadala ya urais huandaliwa na ushirikiano wa mashirika ya habari nchini na hupeperushwa moja kwa moja katika vyombo tofauti vya habari vikiwemo televisheni na redio.

Waandalizi Jumapili walikuwa wametangaza mjadala wa wagombea huru ungeanza saa kumi na moja unusu jioni hadi saa mbili usiku, na maandalizi yote yalikuwa yamekamilika.

Mamilioni ya pesa hutumiwa kuandaa mijadala hiyo na itakuwa pigo na hasara kubwa kwa waandalizi kama Bw Ruto atakosa kufika, kwani watazamaji wengi wangependa zaidi kumweka kwenye uzani na Bw Kalonzo.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako