If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, July 3, 2017

RAILA: VIONGOZI WA JUBILEE NI DOMO KAYA TU

Na SAMMY WAWERU

MUUNGANO wa National Super Alliance (NASA) Jumamosi ulielekeza kampeni zake katika Kaunti ya Bomet kwa minajili ya kuwarai wapiga kura kaunti hii kuchagua kinara wake Raila Odinga katika uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 8.

Bomet Green Stadium
Kinara wa Nasa, Raila Odinga ahutubu katika mkutano wa hadhara Julai 1, 2017 katika kaunti ya Bomet. Picha/BENSON MOMANYI

Kaunti ya Bomet inaongozwa na Gavana Isaac Kiprono Ruto ambaye pia ni kinara katika muungano wa NASA. Kwa mujibu wa sajili mpya ya wapiga kura iliyotolewa na tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC), Kaunti ya Bomet ina wapiga kura 322, 012 ambao muungano wa NASA na mrengo wa Jubilee wanawashawishi wawapigie kura Agosti 8.

Kinara wa NASA Raila Odinga akihutubu katika Kaunti ya Bomet amesuta mrengo wa Jubilee kuwa umeshindwa kutekeleza wajibu wake kama ulivyoahidi kwenye manifesto yake mwaka wa 2013. "Waswahili husema siku za mwizi ni 40, sasa zimesalia siku 38 tuingie debeni tukutane na wao.

 Tofauti yetu na Jubilee ni kama usiku na mchana. Sisi si kama Jubilee waliowaahidi vipakatalishi, kutengeneza barabara, kazi kwa vijana na ahadi zingine nyingi ambazo hamtaziona. Barabara zilizoko hapa tulizitengeza kwenye serikali ya mseto," akasema Raila akihutubu katika Kaunti ya Bomet akiandamana na vinara wenza akiwemo Naibu wake Kalonzo Musyoka.

Kwenye serikali ya mseto iliyoongozwa na Rais Mstaafu Mwai Kibaki, Raila Odinga alikuwa Waziri Mkuu naye Kalonzo Musyoka akiwa Naibu wa Rais.

"Jubilee ni mdomo, mdomo kaya tu. Wanakuja kuzindua miradi wakati ambapo siku 38 pekee zimesalia. Hawa jamaa ni kama wale wanaotaka kuchinja kuku, wanamrushia mahindi kuku anadhani leo amekumbukwa hajui maji yako motoni awe kitoweo," akasema Raila akikejeli serikali ya Jubilee inayoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto.

Jubilee kwenye kampeni zake za kusaka kura kwa ajili ya kuvutia ngoma upande wake waibuke washindi Agosti 8, wamekuwa wakizindua miradi mbali mbali ya maendeleo katika maeneo wanayoenda kuuza sera na ajenda zao huku wakiahidi wapiga kura makuu endapo watachaguliwa.

Raila Odinga kwenye hotuba yake Bomet ameendelea kuuza sera na ajenda za manifesto ya NASA iliyozinduliwa rasmi Jumanne Juni 27.
"Wengi wa vijana hapa wanafanya kazi ya boda boda ambayo si kazi. Ama mnataka kufanya uanaboda boda kwa maisha yenu yote?" akauliza Raila.

"Tunataka kubuni kazi kwa vijana kwa kutekeleza ugatuzi ipasavyo. Kuanzia mwezi Septemba mwaka huu NASA ikichaguliwa, kuanzia chekechea hadi kidato cha nne elimu itakuwa ya bure. Kila kitu kitafadhiliwa na serikali, mtoto kazi yake ni kutoka nyumbani aende shuleni kusoma pekee," alisema Raila akiuza ajenda za NASA.

Wakati wa uzinduzi wa manifesto ya NASA, Musalia Mudavadi ambaye ndiye mkurugenzi wa kampeni za NASA alisema kuwa iwapo muungano huu utachaguliwa Agosti 8, utagatua elimu kando na mfumo wa elimu kuwa wa bure bila malipo kuanzia Chekechea, Shule za Msingi hadi za Pili. Kauli ya Bw Musalia iliungwa mkono na Moses Wetang'ula.

Elimu

UhuRuto wamekuwa wakisuta NASA kuwa hawajiandaa kutekeleza mfumo wa elimu bila malipo.

"Wenzetu tunaoshindana na wao kwa heshima hawakufikiria vile elimu ya bure shule ya upili itakavyoendeshwa. Tulipotangaza kuwa Jubilee tutatoa elimu ya upili bila malipo, kesho yake NASA pia walisema kuanzia Septemba mwaka huu watatoa elimu ya upili bila malipo. Hawajui sisi tulipangia ufadhili wetu wa ajenda hiyo kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita," akasema Rais Kenyatta akihutubu Kaunti ya Kitui Ijumaa Juni 30.

Raila akiwa Bomet ameeleza imani yake kuwa NASA itaibuka washindi uchaguzi mkuu ujao.

"Tulipokuwa hapa awali Gavana Isaac Rutto hakuwa kwenye NASA (Akirejelea mwaka wa 2013), sasa tumerudi hapa akiwa kwenye NASA. Wale jamaa wawili si mnawajua? Mara hii hawana bahati kwa sababu tutawakamatia chini," akasema Raila akilenga Rais Kenyatta na Naibu wake Ruto.

Gavana Rutto mwaka wa 2013 alikuwa akiunga mkono Rais Kenyatta kuchaguliwa japo sasa anaunga mkono kinara wa NASA. Gavana huyu pia ni miongoni mwa vinara wa NASA.

Moses Wetangula akihutubu kwenye kampeni ya NASA Bomet ameitaka tume ya IEBC kuweka wazi na hadharani sajili ya wapiga kura wataoshiriki uchaguzi mkuu ujao.

"Tume ya IEBC Wakenya wanataka kujua usafishaji wa rejista ya wapiga kura mliofanya iko wapi, kwa sababu ukituma ujumbe ili uthibitishe iwapo uko katika sajili ya wapiga kura unapokea mambo mengine," akadokeza Wetangula akieleza baadhi ya masaibu yanayotokana na ujumbe unaopokelewa mpiga kura akithibitisha iwapo yuko kwenye sajili ya wapiga kura ya IEBC. Wafula Chebukati ndiye mwenyekiti wa IEBC.

Wetangula aidha amesuta Naibu Rais Ruto kuwa amekuwa akijigamba kuwa yeye ndiye mbabe wa siasa za Bonde la Ufa.

"Yule jamaa amekuwa akijidai kuwa ameshika watu wa Rift Valley mkono, afungue runinga yake ajionee watu wa Bomet mko ndani ya NASA," akasema Wetangula akisuta Naibu Rais Ruto.

Gavana wa Bomet Isaac Rutto ameahidi wananchi wa kaunti hii kuwa endapo NASA itachaguliwa Agosti 8 itaangazia kikamilifu masaibu ya wakulima wa majani chai. "Hapa Bomet shida ya deni kubwa ya kilimo cha majani chai. Jubilee imetembea hapa na haijaangazia hii shida. Nahakikishia watu wa hapa kuwa NASA ikiibuka washindi Agosti 8, tutaanza kushughulikia wakulima wa majani chai. Majani chai ndio nguzo kuu ya nchi hii," akaeleza Gavana Rutto.

Gavana huyu aidha amekuwa katika mstari wa mbele kupigania ugatuzi nchini hususan alipokuwa mwenyekiti wa Baraza la Magavan nchini (CoG) ambalo sasa linaongozwa na Gavana wa Turkana Josphat Nanok.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako