If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, July 21, 2017

Rais Kabila wa DRC na familia yake wana utajiri wa mamilioni ya dola

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na familia yake wanamiliki hisa katika mashirika 80 nchini humo na maeneo mengine ya dunia na utajiri wake unakadiriwa kuwa makumi ya mamilioni ya dola.

Ripoti iliyotolelwa Alhamisi na Kituo cha Utafiti wa Kongo katika Chuo Kikuu cha New York, Marekani imesema uchunguzi wake kuhusu utajiri wa Kabila umetegemea tu taarifa zilizo wazi kwa umma kama vile hati miliki za ardhi na nyaraka za uanzishaji mashirika. 

Hadi sasa ripoti hiyo ndio kamilifu zaidi kuhusu utajiri wa Kabila na familia yake baada ya miongo miwili ya kuwa rais wa nchi hiyo tajiri kwa madini.

Msemaji wa serikali ya Kongo Kinshasa Lambert Membe amesema, kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo rais hakatazwi kuwa na hisa au kuwekeza katika mashirika mbali mbali.

Kabla ya baba yake Kabila, Laure-Desire, kuingia madakrani mwaka 1997, alikuwa akiishi na familia yake uhamishoni Tanzani ambako taarifa zinasema hali yao ya kifedha haikuwa nzuri. 

Lakini hivi sasa familia ya Kabila ina karibu hekari 70,000 za mashamba ya kilimo, idadi kubwa ya hisa katika shirika kubwa zaidi la simu za mkononi DRC pamoja na leseni zaidi ya 100 za kuchimba dhaharbu na almasi.

Wakimbizi wa ndani ya nchi DRC

Uchunguzi unaonyesha kuwa mashirika hayo yamekuwa na mapatano ya mamilioni ya dola tokea mwaka 2003 huku mali za Kabila na familia yake zikiwa na thamani ya makumi ya mamilioni ya dola. 

Ripoti hiyo haijaashiria akaunti za Kabila na familia yake katika benki mbali mbali nchini humo na maeneo mengine duniani.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako